ASHINDA BILIONI 4 KWA KUBASHIRI (BET) MATOKEO YA MPIRA WA MIGUU

KENYA: Samuel Abisai, amepata bahati ya kujishindia kitita cha jumla ya shilingi za Kenya milioni 221 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 4.8 katika mchezo wa kubashiri kupitia kampuni ya SportPesa.
Mshindi huyo aliyetangazwa siku ya Jumanne katika ukumbi wa ‘Carnivore Restaurant’ ulioko jijini Nairobi alishinda baada ya kubashiri kwa usahihi michezo 17.
Kitita hicho alichokishinda Samwel, kinaweza kutumika kumlipa mchezaji wa Tottenham Hotspur raia wa Kenya, Victor Wanyama kwa muda wa miezi 7 na siku 11.
Siku ya Jumatatu, SportPesa walisema kuwa mshindi huyo aliweka Ksh 200 (TZS 4,338) katika ‘mega jackpots’ mbili akitumia Ksh. 100 kwa kila moja, na walipompigia simu, Samwel alikuwa ametambua kuwa ameshinda tayari na alishaanza kushangilia.
“Samwel alikuwa na wenzake aliobashiri nao wakijadiliana kitu cha watakachofanya na fedha hizo wakati alipopigiwa simu na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Ronald Karauri” walisema SportPesa.
A word from the man of the day!!! Where was he and what was he doing when he learnt of his great fortune? 
Ronald alimshauri Samuel aliyekuwa akishangilia na kupiga makelele, kuacha na kurudi nyumbani na alikubali na kurudi mara moja.
Baada ya kampuni hiyo ya bahati nasibu kutangaza kuwa kuna mshindi wa Ksh. milioni 221 katika mitandao ya kijamii, wakenya wengi walisema kuwa wamehamasika kushiriki mchezo huo wa bahati nasibu katika kampuni ya SportPesa.
Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Twitter waliongeza kwa kusema pesa hizo zinaweza kufanya makubwa na kubadilisha kabisa hali ya maisha ya Samuel.
Ushindi huu umekuja miezi miwili baada ya wakenya wengine wawili kujishindia KSh. milioni 62 kila mmoja katika mchezo huo wa bahati nasibu wa SportPesa.
Hapa chini ni Tweets zilizochapishwa na Kampuni ya Sportpesa wakati wakiwa na Samuel Abisai.
\

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post