BAADA YA KUGOMEA MECHI KATIKA SERIE A, MUNTARI AFUNGIWA MECHI ITALIA

Kiungo wa kati wa Pascara Sulley Muntari, amefungiwa kucheza mechi moja baada ya kulalamikia matamshi ya kibaguzi alipokuwa uwanjani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Italia 'Serie A' , alipewa kadi yanjano baada ya kumuomba refa asimamishe mechi siku ya Jumapili dhidi ya Cagliari akisema kuwa alikuwa akibaguliwa kwa misingi ya rangi.
Mchezaji huyo wa zamani wa Ghana mwenye umri wa miaka 32, baada ya kuzungumza na mwamuzi aliondoka uwanjani hatua iliyosababisha apewe kadi ya pili ya njano.
Mafisa wamesema kuwa siyo mashabiki wengi waliendesha ubaguzi kuweza kuchukua hatua.
Kamati ya Nidhamu ilikubaliana kuwa vitendo hivyo vilikuwa vibaya lakini sera zake haziruhu hatua kuchukuliwa kwa kuwa ni chini ya mashabiki 10 walihusika.
Baada ya adhabu hiyo, aliyekuwa mshambulijia wa Tottenham, Garth Crook anasema kwa kila mchezaji wa Kiafrika katika ligi ya Itaia, anahitaji kugoma wikendi hii iwapo Sulley Muntari hawezi kuondolewa marufuku ya kutocheza mechi moja.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post