BEN POL AWEKA WAZI SABABU ZA KUPIGA PICHA ZA UTUPU

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Bernad Paul maarufu kama Ben Pol, leo amelizungumzia suala la picha zake za utupu zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na kuthibitisha kuwa ni picha zake na kwamba ameziweka kwa lengo maalum.
Akizungumza leo Mei 23, katika kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds fm, Ben Pol alisema kwamba alitumia ustadi wa kuonyesha taswira ya kutekwa (mtu aliyetekwa) kwa mashabiki wake na amefurahishwa kuwa ile taswira aliyotaka kuonyesha imefanikiwa.
“Katika kuonyesha hali ya kutekwa kuna vitu vitatu au vinne ambavyo havitakiwi kukosa katika huo mchoro. Cha kwanza, hiyo picha inatakiwa ionekane kwamba hakuna freedom, hakina power, hakina haki na pia hata hakina privacy, faragha, usiri wala ustaha”
“Kwa hivyo mimi kama Msanii ninayefanya sanaa mwenye ustadi wa kuonyesha mawazo kwa jamii, kwa hadhira, kwa mshabiki nimetaka kuonyesha feeling ya mtu aliyetekwa. Nilitaka kuonyesha taswira ya mtu aliyetekwa. Kwahiyo nilikuwa siwezi kuweka hivyo vitu kimojawapo kati ya hivyo, siwezi kuweka uhuru, siwezi kuweka hali yoyote ya haki au hali yoyote ya privacy kwenye ile picha,” alisema Ben Pol.
“Hata maoni nimeyasoma watu wanasema itakuwa wamehack account yake, itakuwa wamechukua simu yake wanamtesa wanampiga picha bila ridhaa yake,.. Kwangu mimi kama binadamu nasema kuwa hii siyo nzuri, nawaweka watu kwenye presha, lakini kama Artist na management yangu tunagonga cheers tunasema tumeshinda kama art, kama sanaa. Kwa hiyo, hiyo ndiyo taswira niliyotaka kuionyesha,” Aliongeza Ben Pol.
Ben Pol ameeleza kuwa dhumuni hasa la mradi (project) hiyo maudhui yake yanahusu kutekwa na kuwataka mashabiki wake kukaa tayari kuusikia wimbo huo mpya ndani ya saa 24 kutoka sasa.
“Project yangu inayokuja au mradi wangu unaofuata sasa hivi maudhui yake yanahusu kutekwa. Kwa hiyo zile picha unazoziona ni material ya promotion kuelekea kwenye mradi wangu ambao hapa tunapozungumza sasa hivi chini ya masaa 24 watu wataweza kuusikiliza. Kwa hiyo huo wimbo maudhui yake yana feeling ya kutekwa. Kutekwa kuna maana nyingi, inaweza kuwa kutekwa kimapenzi ama kutekwa kwa namna yoyote il…,” Aliongea ben Pol
Ben Pol aliwataka mashabiki wake waelewe kuwa kila kinachoendelea ni planned (kimepangwa) na hakuna makosa yoyote na kuwasihi watambue kuwa amefanya vile kama sehemu ya sanaa kwani  sanaa inahitaji vitu vingi ili kuikamilisha.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post