BREAKING: ALIYEKUWA MBUNGE WA MOSHI MJINI, NDESAMBURO AFARIKI DUNIA

KILIMANJARO: Aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Philemon Ndesamburo amefariki dunia leo Mei 31, 2017.
Ndesamburo ambaye alikuwa miongoni mwa wanasiasa wakongwe nchini na pia Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro , amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi.
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kueleza kuwa taratibu nyingine za maziko zitafuata.
Ndesamburo ameliongoza jimbo la Moshi Mjini kwa vipi vitatu mfululizo kuanzia mwaka 2000 hadi 2015.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post