BREAKING: MATOKEO YA UCHAGUZI WA WABUNGE WA CHADEMA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Bunge la Tanzani Jana limepiga kura na kuwachagua wabunge wawili wa CHADEMA watakaoungana na wenzao 7 kutoka CUF na CCM kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Uchaguzi huo wa wabunge wa CHADEMA umerudiwa jana baada ya wagombea wa kwanza kukataliwa bungeni kwa kupigiwa kura ya hapana kwa kile kilichoelezwa kuwa hawakuwa wamekidhi vigezo.
Katika uchaguzi wa jana, wabunge wawili waliochaguliwa ni  Josephine Sebastian Lemoyan na Pamela Pamela Maasay.
Katika kinyang’anyiro hicho wagombea wengine walikuwa nia Ezekiel Wenje, Lawrence Masha, Salum Mwalimu na Prof. Safari.
Kufuatia ushindi wa wagombea hao wawili, wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki sasa wanafikia 9 ambapo 5 ni wanawake na 4 ni wanaume.
Wabunge tisa wa Tanzania katika Bunge las Afrika Mashariki ni;
  1.  Fancy Nkuhi (CCM)
  2. Happiness Legiko (CCM)
  3. Maryam Ussi Yahya (CCM)
  4. Dkt Abdullah Makame (CCM)
  5. Dkt Ngwaru Maghembe (CCM)
  6. Alhaj Adam Kimbisa (CCM)
  7. Habib Mnyaa (CUF)
  8. Josephine Sebastian Lemoyan (CHADEMA)
  9. Pamela Pamela Maasay (CHADEMA).
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post