BREAKING: VIDEO YA GIGY MONEY YASABABISHA ABERT MSANDO KUJIUZULU ACT WAZALENDO

Aliyekuwa Mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo na mwanasheria mashuhuri, Albert Msando amejiuzulu nafasi hiyo kufuatia mkanda wa video unaomdhalilisha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Kupitia mitandao ya kijamii, ilisambaa video ikimuonyesha kiongozi huyo akiupapasa mwili wa Gigy Money na kwamba kujuzulu kwake ni kuonyesha kujutia na pia kuwajibika kutokana na kitendo hicho ambacho siyo cha maadili mema ya kiongozi.
Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe amesema kuwa Msando ameandika barua ya kujiuzulu na ameomba msamaha na wao kama viongozi ni wajibu wao kumsamehe na kumsaidia kupita katika mitihani inayomkabili. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto Ameandika.
Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo.
Ndugu Msando anawajibika Kwani anapaswa, nannukuu kutoka katika barua yake, “kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka”.
Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama.
Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake.
Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama – ACT Wazalendo
Dar es salaam
Mei 23, 2017
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post