BREAKING: WAZIRI MWAKYEMBE APIGA MARUFUKU VYOMBO VYA HABARI KUSOMA MAGAZETI ASUBUHI

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harrison George Mwakyembe amevipiga marufuku vyombo vya habari nchini (runinga na redio) kusoma habari nzima zilizomo kwenye magazeti.
Waziri Mwakyembe amesema kuwa marufuku hiyo inaanza kesho kwamba vyombo vya habari havitatakiwa kuisoma habari yote kama ilivyoandikwa kwenye gazeti.
Akieleza dhumuni la marufuku hii, Waziri Mwakyembe amesema ni ili magazeti yaweze kuuza kwani ukishasoma habari yote kwenye chombo cha habari na watu wakasiliza maelezo yote hakuna mtu atakayenunua gazeti hilo tena.
Kauli hii ya waziri imekuja wakati dunia ikiadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo Tanzania imeshuka kwa nafasi 3 katika orodha ya uhuru wa habari, hii ikichangiwa na uwepo wa sheria ya makosa ya mitandao, sheria ya huduma za habari pamoja na kutishwa, kujeruhiwa au kufungwa kwa waandishi wa habari.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post