CCM WAHEPA KONGAMANO LA VIGOGO WA UKAWA

Vigogo wa CCM wakwepa kuhudhuria kongamano lililolenga kujadili kuhusu demokrasia ilipotoka, ilipo na ilnapokwenda, lililoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kongamano hilo lililenga kuwahusisha viongozi mbalimbali kutoka Chama cha Mapinduzi akiwemo katibu Mkuu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey polepole.
Vile vile lingewahusisha viongozi wengine wanaotoka katika vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Chama cha Mapinduzi kupitia taarifa waliyoisambaza katika mitandao ya kijamii kiilieleza kuwa chama hakijapata mwaliko wa kongamano na hata viongozi wanaotajwa katika tangazo lililoenea mitandaoni hawana taarifa.
“CCM inathamini mijadala, midahalo na makongamano yenye lengo la kupeleka ajenda za maendeleo ya wananchi wetu mbele ambayo yanaandaliwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu,” inasema taarifa hiyo ambayo inaonekana kusainiwa na Polepole.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post