CHELSEA IMEDHAMIRIA KUTWAA UBINDWA LIGI KUU YA UINGEREZA

Vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea wamepiga hatua kubwa katika kuelekea kutwaa ubingwa baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Everton katika dimba la Goodison Park.

Chelsea ilipata goli la kwanza kwa shuti kali la Pedro la umbali wa yadi 25, kisha Gary Cahill alifunga la pili kwa shuti la karibu kabla ya Willian kufunga la tatu na kuifanya iendelee kuongoza kwa tofauti ya pointi nne.

Kwa ushindi huo Chelsea hata wakipoteza pointi tatu katika michezo minne iliyosalia bado wataweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, hata kama Tottenham watashinda michezo yote iliyosalia.
                                    Pendro akiachia shuti kali lililozaa goli la kwanza la Chelsea
                                      Gary Cahill akiifungia Chelsea goli la pili katika mchezo huo 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post