CHINA YARUSHA NDEGE YAKE YA KWANZA ILIYOTENGENEZWA NCHINI HUMO

Ndege kubwa ya abiria ya kwanza kutengenezwa nchini China imefanya safari yake ya kwanza na kuibua changamoto kwa kampuni kubwa za utengenezaji ndege za Boeing na Airbus.

Televisheni ya taifa ya nchi hiyo imeonyesha ndege hiyo iliyotengenezwa na shirika la umma la China ikiruka bila tatizo lolote ikitokea uwanja wa ndege wa Pudong uliopo Jijini Shanghai.

Ndege hiyo ni hatua muhimu kwa China, katika hamasa yake ya kutinga katika soko la dunia kwa uuzaji ndege.


Shirika hilo la Comac lilipanga tangu mwaka 2008 kuitengeneza ndege hiyo lakini mpango huo ulikuwa ukisogezwa mbele kwa muda wote huo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post