DARASSA KUACHIA NGOMA MPYA LEO KAA MKAO WA KULA

Hit maker wa nyimbo iliyokua anthem, ‘Muziki’, Darassa aka ‘CMG’, Alhamisi hii anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao Hasara Roho.

Rapa huyo ameanza siku kwa kuwashukuru mashabiki wake kwa ushirikiano waliomwonyesha katika project yake ya wimbo ‘Muziki’.
“Good morning from Bongo Tanzania East Africa to the Top of the world!. Nataka kusema asanteni sana kwa love na support ambayo mmetupatia kwenye project yetu ya  ‘Muziki’ na  kuipelekea kuwa National Anthem. Hakuna neno linaweza kumaanisha thamani yenu kwetu! God bless you all usikose kusikiliza project yetu mpya leo ๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™ #CMG#HasarARoho,” aliandika rapa huyo Instagram.
Mmoja kati ya mameneja ambao wanafanya kazi na rapa huyo, Hanscana,hivi karibuni aliiambia Bongo5 kuwa ujio mpya wa rapa huyo umeandaliwa kama anavyoandaliwa mtu anayekuja kuwa Rais wa nchi.
“Sisi tumejiandaa vizuri kwa sababu tunajua mashabiki wanataka nini. Maandalizi ni makubwa sana, yaani ni kama tunaandaa Marais 5 wa nchi. Kwahiyo tumejipanga vizuri kuhakikisha jamaa anarudi vizuri katika game,”
Video ya wimbo ‘Muziki’ wa rapa huyo imeangaliwa mara 7,056,225 kwa kipindi cha miezi 5 tu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post