DIAMOND AITAJA KAZI AMBAYO HATAKI MTOTO WAKE WA KIKE AIFANYE

Mwanamuziki Diamond Platnumz amesema kuwa angependa kumuona mtoto wake wa kiume, Nillan anakuwa msanii kama yeye lakini asingependa mwanae wa kike, Tiffa awe msanii.
Diamond alieleza sababu za kutotaka mtoto wake wa kike kuwa msaani kwamba anahofia sana wanaume kumtumia kwenye masuala ya kuajamiiana kutokana na yeye kuwa maarufu.
Diamond aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kupitia kipindi cha The Trend kinachoongozwa na Larry Madowo.
Mtu akishakuwa msanii, na idadi ya watu wanaomfahamu inaongezeka, hivyo wanaume wanaomtongoza nao wanaongezeka, kitu ambacho kitanitia presha kujua kwamba mwanangu ametembea na wanaume wengi, alisema Diamond
Mbali na wanae, Diamond pia alimsifia mzazi mwenzake, Zarinah Hassan na kusema ni mwanamke mwenye kujielewa sana, anayefahamu kuhusu kesho, na hivyo anamshukuru Mungu sana kwa kumpata na kumzalia watoto.
Unaweza kutazama mahojiano yote hapa chini.JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post