DIAMOND PLATNUMZ AMSAINISHA MSANII MWINGINE WCB

Msanii Diamond Platnums leo kupitia lebo yake ya WCB Wasafi anatarajia kumtangaza msanii mpya atakayejiunga na kufanya kazi chini ya lebel hiyo.
Diamond ameyaeleza hayo kupitia ukurasa wake katika mtandao wa instagram na kuwaomba watanzania kuendelea kuisaidia na kuwa karibu na WCB Wasafi kwani siyo ya kwake tu, bali ni ya mashabiki wake pamoja na wananchi wote.
Panapo majaaliwa siku ya jumatatu kesho, ntakuwepo kwenye LEO TENA ya Clouds fm na familia nzima ya @Wcb_wasafi tukimtambulisha Kijana mwenzetu Mwingine Mpya toka Mtaani, ndani ya @Wcb_Wasafi….. Sisi ni vijana ambao tumekulia kwenye umaskini na bado tupo kwenye kupambana namna ya kujikwamua kwenye umasikini… na ndiomaana tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kila tukiona kijana yoyote mwenye nia na kipaji kumsaidia kwa kadri ya uwezo wetu, ili nae aweze kutambulisha kazi zake, na Pengine Mwenyez Mungu akimjaalia nae awe mkombozi kwenye Familia yake….Sio jambo Rahisi ni gumu, lakini kwa Sapoti yenu naamini tunaweza lifanikisha…Siku zote naomba mkumbuke WCB_Wasafi sio ya Diamond, ni ya vijana wote wapambanaji…na ndiomaana kila siku nawaomba Muendelee kuniombea na Kunisapoti, kwani Sapoti yenu ndio itayo nifanya hata kesho niweze kukuchukua wewe ama ndugu yako ili aje kukitambulisha kipaji chake na Mwenyez Mungu akijaalia kufikia Malengo…… USIKOSE kusikiliza Leo tena ya @Cloudsfmtz saa nne Asubuhi…Shukran๐Ÿ™
Vile vile aliwasihi vijana wote kuendelea kupambana kutafuta namna ya kujikwamua kutoka kwenye umasikini ili waweze kujikomboa wao pamoja na familia zao na kuiletea nchi yetu maendeleo.


JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post