FAHAMU JINSI YA KUPUNGUZA UZITO KWA KUTUMIA NDIZI MBIVU

Kuna watu huwa na mtazamo wa tofauti dhidi ya tunda la ndizi kwamba husababisha mtu kuwa na mafuta mengi mwilini. Hii siyo kweli na ni kwamba tunda hili ni la maajabu na lina zadi ya ambavyo kila mtu anavyofikiri kulihusu.
Jambo zuri ni kwamba tunda hili linapatikana muda wote katika mwaka na huwa siyo gharama sana kulipata.
Ni chanzo kizuri cha madini, vitamini katika mwili na ni tamu pia. Hizi hapa ni baadhi ya faida za kiafya zipatikanazo katika ulaji wa ndizi mbivu.
Hukusaidia kuwa na nywele zenye afya.
Kama unapenda kuepukana na kemikali zinazopatikana katika bidhaa za nywele za viwandani unazonunua, basi unaweza kujitengenezea mwenyewe mchanganyiko wa ndizi ambao utakufanya uwe na nywele zenye muonekano mzuri. Ndizi zina Vitamin- B na ‘folate’ ambazo huzifanya nywele kuwa na muonekano wa kuvutia.
Changanya ndizi mbivu , maziwa pamoja na asali, kisha paka mchanganyiko huo katika nywele zako na uziache kwa muda wa dakika 20, halafu uzioshe na kuzikausha vizuri. Matokeo yake yatakushangaza hakika.
Ukitaka ngozi yako iwe nyororo na yenye kung’aa, basi ponda ponda ndizi kisha uzipake katika uso wako. Kaa nazo kwa muda wa dakika 15 halafu uoshe uso kwa maji baridi.
Ndizi mbivu huwa inang’arisha ngozi yako kwa kuwa ina vitamin A inazuia kubadilika rangi ya ngozi pamoja na vitamin E inayoilinda ngozi dhidi ya mabaka.
Ndizi hupunguza kiwango cha wasiwasi.
Ndizi mbivu zina kiwango kikubwa cha ‘potassium’ kinachosaidia kupunguza mawazo. Hii hutokea kwa kuwa ‘potassium’ hudhibiti kiwango cha homoni za mawazo “stress hormones” katika mwili wako.
Ndizi huweza pia kuongeza kiwango cha utendaji kazi cha akili yako, Hivyo jaribu kula ndizi kabla ya kufanya mkutano, ‘presentation’ au vikao kwa kuwa itakusaidia kupunguza kiwango cha wasiwasi na kuongeza ufanisi wa akili yako katika kuyafanya majukumu yako ya kila siku.
Ndizi mbivu huchochea kupungua kwa uzito wa mwili.
Nina uhakika watu wachache wanajua kuhusu hili, lakini wengi hawaujui ukweli kuwa ndizi husaidia sana katika kupunguza uzito wa mwili. Husaidia mwili wako kuchoma kalori “Burn calories’ . Ndizi moja ya wastani, inakuwa na kalori 105. Vile vile zina madini ya ‘chorium’ yanayousaidia mwili wako kuchoma kalori ambazo huwa zikilundikana mwilini husababisha uzito wa mtu kuongezeka.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post