HALI YA MBUNGE WA CHADEMA MATATANI, ALAZWA MUHIMBILI

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jana akitokea Dodoma kwa ajili ya matibabu baada ya kyzidiwa ghafla.
Mbunge huyo anasumbuliwa na  uvimbe ambapo mdogo wake, Edward Heche amesema kuwa kaka yake alianza kupatwa na maumivu makali juzi (Jumatano) akiwa Dodoma ndipo alipokwenda kwa ajili ya kumsaidia.
“Nilifika Dodoma saa tisa nikamkuta anatibiwa katika Hospitali ya Bunge hali yake haikuwa nzuri alikuwa analalamika kuwa maumivu yalizidi, tukampelekea Hospitali ya Mkoa bado aliendelea kulalama huko akapewa dawa za kupunguza maumivu lakini haikusaidia tulipoandikiwa kuja Muhimbili,” amesema na kuongeza;
“Hali ya Heche sio nzuri, tatizo ni kwamba alifanyiwa upasuaji kwenye uvimbe uliokuwa pajani lakini kwa bahati mbaya inaonekana baadhi ya nyuzi ziliachia na ndiyo inamsababishia maumivu makali.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post