HALI YA WATOTO MAJERUHI WA LUCKY VICENT YANDELEA KUIMARIKA

Hali ya watoto majeruhi walionusurika katika ajali ya basi huko Rhotia Wilaya ya Manyara, mkoani Arusha na kupelekwa nchini Marekani kwa ajili ya matibabu. imeendelea kuimarika.
Mbunge wa jimbo la Singida, Lazaro Nyalandu kupitia ukurasa wake wa ‘instagram’ leo ameandika akieleza kuwa maandalizi ya wali ya kuwapeleka watoto hao katika makazi maalum kwa ajili ya kuendeleza uangalizi pamoja na kufanyishwa mazoezi yameanza, ingawa watabaki katika Hospitali ya Mercy mpaka madaktari watakapojiridhisha na hali yao.
“MADAKTARI wa Mercy hospital WAMESEMA WATOTO wote watatu Wilson, Doreen, na Sadia wameendelea VEMA, na maandalizi ya awali yameanza ya kuandaa kuwapeleka “Special Rehab”, au Makazi Maalum ya kuendeleza uangaliza wa KARIBU wa AFYA zao, na kufanyiwa MAZOEZI, ingawa wataendelea KUWA WODI ya WATOTO Mercy Hospital kwa SASA hadi MADAKTARI bingwa WATAKAPOJIRIDHISHA na hali yao. MTOTO Wilson alinukuliwa na VYOMBO vya HABARI vya America akisema “Thank you”. MTOTO Sadia aliseme “Hello TANZANIA”. Sote TUENDELEE kuwaombea. MUNGU mwenyewe AKAWATENDEE mema kwa UTUKUFU wake.
(Kutoka Siouxland-proud)”

A POST SHARED BY LAZARONYALANDU (@LAZARONYALANDU) ON 
Nayo Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo imetuma jumla ya shilingi milioni 44 nchini Marekani kuwawezesha wazazi wa watoto hao pamoja na daktari na muuguzi walioongozana nao.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post