HARRY KANE AFUNGA MAGOLI MANNE WAKATI TOTTENHAM IKIICHAKAZA LEICESTER CITY

Harry Kane amefunga magoli manne wakati Tottenham ikitakata na kuichakaza vibaya timu ya Leicester City kwa magoli 6-1.

Licha ya kupoteza matumaini ya kutwaa ubingwa wiki iliyopita kikosi hicho kinachonolewa na kocha Mauricio Pochettino kilihakikisha kinashinda mechi 25 katika msimu huu.

Katika mchezo huo Kane alifunga magoli mawili akiwa karibu na goli na magoli mengine mawili akiwa umbali wa yadi 20 na kufikisha magoli 26 katika msimu huu.

Mkorea Kusini Son Heung-min naye alifunga magoli mawili mazuri moja katika kila kipindi huku Dele Alli akifunga baada ya kupatiwa pasi nzuri.
                                  Harry Kane akifunga goli lake la kwanza katika mchezo huo
                                              Son Heung-min akipachika goli la pili la Tottenham

                                        Harry Kane akifunga goli lake la pili katika mchezo huo
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post