HARRY KITILYA NA WENZAKE WATAKA UPELELEZI UKAMILIKE

Aliyekuwa Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Msamire Kitilya (katikati) mshindi wa Mashindano ya Urembo (Miss Tanzania), mwaka 1996, Shose Mori Sinare (kulia) na Sioi Graham Solomon (kushoto).
UPANDE wa utetezi katika kesi inayomkabili Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Msamire Kitilya,mshindi wa Mashindano ya Urembo (Miss Tanzania), mwaka 1996, Shose Mori Sinare na Sioi Graham Solomon, wameuomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo.
Hayo yalielezwa leo na wakili wa utetezi Majura Magafu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kisutu, Cyprian Mkeha baada ya Wakili wa Serikali, Patrick Mwita kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Majura alidai kuwa wanauomba upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha upelelezi wa kesi hiyo haraka ili kuendelea na hatua nyingine.
Hata hivyo, Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 19 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa Dola za Marekani 550 milioni kwa serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post