HATUA ZA KUCHUKUA MAJI YANAPOINGIA KWENYE MFUMO WA MAFUTA WA GARI LAKO

Mafuta ni kimiminika muhimu kuliko vitu vyote katika gari. Ili gari liweze kufanya shughuli zake zilizokusudiwa lazima liwe na mafuta. uwepo wa mafuta hulifanya gari kutekeleza majukumu yake kama vile kuwezesha mifumo mbalimbali ya gari kufanya kazi kwa ufasaha na kulifanya gari kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Mfumo wa mafuta ni mfumo muhimu sana katika gari ambapo huanzia katika tenki (fuel tank) mpaka katika injini ambako ndiko katika matumizi yake. kazi kubwa ya mafuta ni kukamilisha muwako katika pigo la nguvu (power stroke).
Yapo mambo mbalimbali yanayosababisha mfumo wa mafuta katika gari kupata matatizo na hivyo kusababisha kuharibika au kufa kabisa kwa mfumo huo.
Mambo hayo ni kama vile, maji kuingia, kuharibika kwa chujio la mafuta (fuel filter), pampu ya mafuta kushindwa kufanya kazi, pamoja na mengine mengi.
Baada ya kugundua mfumo wa mafuta katika gari lako una hitilafu, hasa ya kuingiliwa na maji au mafuta yasiyo sahihi, kwa mfano mfumo wa Diesel halafu ukaingiliwa na mafuta ya petroli, au mfumo wa petroli ukaingiliwa na mafuta ya diesel, unatakiwa kufuata hatua zifuatazo ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo.
Kusitisha matumizi ya gari hiyo.
Unashauriwa kusitisha matumizi ya gari yako kama utagundua tatizo kama hili limejitokeza kwenye mfumo wa mafuta. Kama gari linatumia mfumo wa mafuta wa petroli basi utambue kuwa vifaa vyote ni maalum kwa mafuta ya petroli tu. Iwapo linatumia mfumo wa diesel au maji yameingia kwenye mfumo, ni lazima itaketa athari ndiyo maana inakupasa kusitisha matumizi haraka.
Kusafisha mfumo mzima.
Pia unashauriwa kusafisha mfumo wa mafuta katika gari yako kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hili. Hapa saa ni katika hatua ya kutibu tai=tizo moja kwa moja.
Sehemu muhimu ya kuzingatia katika kusafisha mfumo huo ni kama ifuatavyo:-
Kusafisha tenki. tenki husafishwa kwa maji na baada ya hapo husafishwa na mafuta na mwisho hukaushwa kwa muda kabla ya matumizi kuanza upya.
Kusafisha pampu. Kusafisha njia zote za mafuta, badili chujio zote za mafuta (fuel filter), safisha injection/ caburetor pamoja na kubadilisha nozzle.
Tatizo lingine linaloweza kulikumba gari lako, ni tatizo la misfiring. tatizo hili husababishwa na hitilafu katika mfumo wa mafuta kwenye gari.
Misfiring ni kitendo kinachotokea baada ya baadhi ya cylinder zilizopo ndani ya injini kutopata moto sawa sawa, kitendo hiki husababishwa na muingiliano wa hewa na mafuta kwenye chumba cha muwako (combustion chamber). Kitendo hiki husababisha madhara kama vile gari kuzima mara kwa mara, kupoteza nguvu yake ya kawaida pamoja na gari kutetemeka mithili ya gari lililoharibika.
Kwa usalama wa gari lako punde tu baada ya kuona au kuhisi tofauti katika gari lako chukua hatua za haraka kama ifuatavyo:
  • Unapoingiza gari lako katika maji, hakikisha shimo siyo kubwa na upite taratibu bila haraka.
  • Unapotaka kuweka mafuta jitahidi kuweka mafuta bora na si ya wasiwasi wa kuchanganywa, hivyo jitahidi ununue katika kituo sahihi cha mafuta na siyo kununua kwa wanunuzi wa vichochoroni yasiyo na uhakika.
  • Epuka kutumia mafuta yote katika gari mpaka likakuzimikia kwa kukosa mafuta. tabia hii huharibu mfumo wa mafuta na kuua pump ya gari kwa kulazimisha kunyonywa kwa uchafu ulioko ndani ya tenki la mafuta.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post