HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI YAHARIRIWA

Dodoma. Hotuba ya kambi ya upinzani imehaririwa kwa maelekezo ya Spika, Job Ndugai na kuondoa maneno kwenye kurasa namba 4, 7 na 19.
Kabla Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema Lema hajaanza kusoma hotuba hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga amesoma maelekezo ya Spika kuwa maneno hayo yafutwe na yasisomwe kwa sababu yalikwishazuiliwa katika hotuba zilizotangulia.
Alipofika kwenye maneno hayo akaanza kusema "Tatizo la rushwa..., amezimiwa kipaza sauti na kuelezwa na Giga kuwa suala hilo limeondolewa.”
Wabunge kadhaa walitaka kuomba mwongozo wa utaratibu lakini mwenyekiti akawakatalia.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post