HOTUBA YA ZITTO KABWE (MB) KUHUSU BAJETI YA WIZARA YA KILIMO 2017/18

SHARE:

Hotuba ya ndugu Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto (MB) kuhusu Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2017/18 Mheshimiwa Spika, ...

Hotuba ya ndugu Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto (MB) kuhusu Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2017/18
Mheshimiwa Spika,
Serikali yeyote makini lazima ihangaike na masuala yanayowahusu wananchi wake walio wengi, na hapa Tanzania watu hao (walio wengi) ni Wakulima. Hivyo basi, kipimo kikuu cha kuondoa umasikini wa Watanzania ni kuondoa umasikini wa wakulima.
Sekta ya kilimo ndio msingi wa Uchumi wa watanzania. Waziri wa kilimo katika hotuba yake hapa ametuambia kuwa 65.5% ya watanzania wameajiriwa kwenye kilimo au wanategemea kilimo kwa kipato chao cha kila siku, kwamba 100% ya chakula nchi inategemewa kutoka kwenye sekta hii. Kilimo kinachangia 29.1% ya pato la taifa (GDP), karibia theluthi moja ya thamani yote ya shughuli za Uchumi nchini kwetu.
Hivyo basi, unapowekeza kwenye sekta ya kilimo unawekeza kwa theluthi mbili ya watanzania. Unapokuza kilimo unakuza uchumi wa theluthi mbili ya watanzania, na unapoacha kilimo kishuke maana yake umewafukarisha theluthi mbili ya Watanzania.
Kwa mujibu wa wataalamu wa Uchumi, ili kupunguza umasikini Tanzania kwa kiwango kikubwa, sekta ya kilimo inapaswa kukua kwa asilimia zaidi ya 8% angalau kwa miaka mitatu mfululizo, na ukuaji huo uendelee kukua kwa wastani wa 6% kwa muda miaka kumi mfululizo.
Hali ikoje nchini? Kwa mujibu wa hotuba ya Waziri wa Kilimo, kwa miaka hii mitatu mfululizo ukuaji wa Kilimo umekuwa ukishuka nchini (Na hivyo ukuaji zaidi wa umasikini). Mwaka 2014 sekta ya Kilimo ilikua kwa 3.4%, Mwaka 2015 Kwa 2.3% na Mwaka 2016 Kwa 2.1%.
Taarifa ya ya robo mwaka ya Benki Kuu nchini (BOT quarterly economic bulletin) inayoishia Disemba 2016 inaonyesha tofauti na anachosema Waziri. Kwa mujibu wa tarifa ya BOT ni kuwa sekta ya Kilimo ilikua kwa kasi ya 0.6% tu kutoka ukuaji wa 2.3%. 65.5% ya Watanzania wote wamejiajiri katika sekta ya Kilimo, hivyo mdororo huu ya sekta ya Kilimo kutoka ukuaji wa 2.5% mpaka ukuaji wa 0.6% ni ishara mbaya mno kwa ustawi wa zaidi ya robo tatu ya Watanzania.
Kwa Vijijini 78% ya Watanzania wanajihusisha na Kilimo. Hii maana yake ni kwamba wananchi wengi vijijini hawafanyi uzalishaji, jambo hili ni hatari sana, ni dalili kuwa ufukara wa watu wetu unazidi. Ni kwa sababu hii, pamoja na uchumi wetu kukua kitakwimu, 7% kwa mwaka, lakini bado wananchi wetu walio wengi wanaishi kwenye dimbwi la ufukara. Maana ukuaji huo wa Uchumi hauhusishi kilimo, hauhusishi zaidi ya robo 3 ya Watanzania.
Tunajenga uchumi unaowaacha pembeni theluthi 2 ya watanzania wote. Ukuaji huu mdogo wa Kilimo unapaswa kuishtua Serikali kwani ni hatari sana, ni hatari mno. Maana unajenga uchumi unaowaacha karibu zaidi ya robo 3 ya Watanzania kwenye ufukara huko vijijini, ni uchumi unaopanua matabaka ya mafukara na matajiri. Ndio msingi wa umasikini wa wananchi wetu miaka 50 baada ya Uhuru.
Tatizo hasa ni nini? Kwanini ukuaji wa kilimo unashuka na hivyo umasikini wa Watanzania kuzidi? Tatizo kubwa ni sera za Serikali pamoja na utekelezaji wake. Serikali haiwekezi vya kutosha kwenye kilimo, Na hata ikipanga mipango juu ya kilimo haitekelezi kabisa mipango husika.
Katika bajeti ya mwaka 2015/16, bajeti ya mbolea ya Ruzuku katika Wizara hii ilikuwa ni shilingi bilioni 78. Bajeti ya kwanza ya Serikali ya awamu ya tano ilishusha fedha za ruzuku ya mbolea mpaka Shilingi bilioni 10 katika mwaka wa Fedha wa 2015/16. Hii ilikuwa ishara ya dhahiri ya kukipuuza kilimo, kuwapuuza 65.5% ya Watanzania wote, kutokujali chanzo cha 100% ya chakula chote cha Watanzania, kupuuza sekta inayochangia theluthi moja ya uchumi wa Taifa.
Si hivyo tu, katika bajeti ya mwaka 2016/17, Bunge liliidhinishia Wizara hii fedha za miradi ya maendeleo katika kilimo kiasi cha bilioni 100.53. Waziri amelieleza bunge hapa kuwa mpaka Mei 4, 2017 Wizara imepokea shilingi bilioni 3.34, sawa 3.31% ya fedha zote za maendeleo ya kilimo. Jambo hili linasikitisha mno, ni jambo linaonyesha kuwa hatuwajali wanyonge wa Taifa hili.
Watanzania wanyonge walikuwa na matumaini makubwa sana na Serikali hii, Rais Magufuli alisema yeye ni rais wa wanyonge. Wanyonge nchi hii ni wakulima. Matendo ya Serikali anayoiongoza yanaonyesha tofauti, Serikali haiwajali wanyonge, inapuuza uchumi wa 65.5% ya wananchi wetu. Ni vigumu kuondoa umasikini nchini ikiwa tutaendelea kuwadharau wakulima.
Kwetu sisi ACT Wazalendo tunaofuata Ujamaa wa Kidemokrasia, Kilimo ndio sekta ya msingi, ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa, ni sekta nyeti ambayo hatutaacha kuisemea. Hivyo pamoja na kuonyesha kasoro zote hizo za serikali, tutatumia pia nafasi hii kutoa njia mbadala za kuondoa kasoro hizo ili kuhakikisha uchumi wetu hauwaweki kando wananchi wetu wengi.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge – Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)
Bungeni Dodoma
Mei 20, 2017

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,266,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3256,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,329,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,345,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1365,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1280,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,131,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: HOTUBA YA ZITTO KABWE (MB) KUHUSU BAJETI YA WIZARA YA KILIMO 2017/18
HOTUBA YA ZITTO KABWE (MB) KUHUSU BAJETI YA WIZARA YA KILIMO 2017/18
https://3.bp.blogspot.com/-xhGnCNjvZaY/WSFnB_HSghI/AAAAAAAAbog/4BwO02lDbk4hFdJTXxrBCqa6SkIoXpZmwCLcB/s1600/xZITTOKABWE-689x375.jpg.pagespeed.ic.X7uS-pjOnP.webp
https://3.bp.blogspot.com/-xhGnCNjvZaY/WSFnB_HSghI/AAAAAAAAbog/4BwO02lDbk4hFdJTXxrBCqa6SkIoXpZmwCLcB/s72-c/xZITTOKABWE-689x375.jpg.pagespeed.ic.X7uS-pjOnP.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/hotuba-ya-zitto-kabwe-mb-kuhusu-bajeti.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/hotuba-ya-zitto-kabwe-mb-kuhusu-bajeti.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy