JAMBAZI MREMBO NCHINI KENYA AUAWA NA POLISI

Jeshi la polisi Kenya limewauwa kwa kuwapiga risasi majambazi wawili mmoja wao akiwa ni jambazi wa kike anayesemekana kuwa ni jambazi mrembo pengine kuliko wote.
Majambazi hao waliuwawa wakiwa katika eneo la Chokaa Jijini Nairobi walipopambana na polisi kwa kufyatuliana risasi, huku wenzao wawili wakifanikiwa kutoroka.
Mitandao ya jamii imemtambua jambazi huyo mwanamke kwa jina la Claire Mwaniki, ambaye alifariki akiwa ameshikilia bastola mkononi aina ya Baretta ikiwa na risasi sita.
Kwa mujibu wa Polisi, msichana huyo ameolewa kwa mwanaume ambaye naye ni jambazi sugu anayetafutwa na Polisi.
Kamanda wa Polisi Jijini Nairobi, Japheth Koome, amesema kuwa wahalifu wengi nchini humo wanakuwa na wanawake wanaofanyanao ujambazi. Wakati mwingine wanawake hao hutumiwa katika kusafirisha silaha au kukusanya taarifa kutoka maeneo mbalimbali ambayo wamepanga kufanya ujambazi.
Afisa huyo wa Polisi alisema kuwa ushiriki wa wanawake katika ujambazi unaleta changamoto kubwa kwenye usalama kutokana na Polisi kutoruhusiwa kupekuwa pochi za wanawake.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post