JE, WEWE NI MWATHIRIKA WA KUTAZAMA PICHA ZA NGONO? NA UNATAKA KUACHA SOMA HAPA

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kurasa za mitandao ya picha za uchi vimejazwa na matangazo ya dawa za aina mbalimbali za Viagra, ambazo kiuhakika zilitengenezwa kwa ajili ya wazee ambao wanayo matatizo yanayohusiana na kusimamisha uume wao kutokana na kusinyaa au kuzibika kwa mishipa yao ya damu inayotiririka kuelekea kwenye uume. Leo hii vijana wadogo kabisa wanao tembelea kurasa hizo za uchi kwenye mitandao kwa idadi kubwa sana wamekuwa na tatizo la ED, na taarifa zisizo sahihi ni kwamba eti vijana hao wanalo tatizo kwenye viungo vyao vya uzazi, lakini hapana, tatizo lipo kwenye vichwa vyao … ni mara chache sana wanaweza kuongeanisha tatizo hilo na filamu za uchi wanazo tizama kila siku ...”

Kama wewe ni mtizamaji mkubwa wa filamu za uchi, kiasi kwamba siku haipiti au wiki haipiti bila kutazama filamu hizo, na huwezi kujizuia kutazama filamu hizo pale ashki ya kutazama inapokujia na matokeo yake ni kuwa sasa jogoo wako hawezi kuwika mbele ya mtete na sasa unalo tatizo linaloitwa ED (Erectile Dysfunction), kwa maneno mengine ni kuwa ubongo wako sasa hauwezi kupata msisimko wa ngono kutoka kwenye mazingira halisi, unatakiwa sasa kubadilisha njia unayo kwenda kabla hujafika kwenye kona mbaya zaidi katika maisha yako ya ndoa na mwenza wako.
Njia ya kuiokoa ndoa yako, au maisha yako ya baadaye kwenye ndoa ni safari ndefu na fupi kutegemeana na muhusika na kipi kitaweza kufanya kazi kwako haraka kurudi kwenye hali yako ya kawaida.
Ubongo wako unapaswa kurudishwa katika hali ya kawaida. Kumbuka ni matumizi ya picha za uchi kwenye mtandao ndiyo yaliyo badilisha namna ubongo wako unavyo fanya kazi katika jambo zima la tendo la ngono, ubongo wako umesukumwa na picha hizo na kufikia kiwango cha juu cha msisimko wa ngono ambacho hakipatikani kwenye mazingira halisi, isipokuwa kwenye mitandao ya ngono, sasa unapaswa kufanya kazi ya ziada kuurudisha ubongo wako katika hali ya kawaida, katika msisimko wa kawaida wa ngono kwenye mazingira halisi. Kumrudishia jogoo wako uwezo wake wa kuwika tena itahusisha vitu viwili kwa pamoja.‘REBOOTING’ na ‘REWIRING’.
Rebooting inamaanisha kuurudishia ubongo wako uwezo wake wa kawaida wa kutiririsha damu ya kutosha kwenye mishipa inayo elekea na iliyopo kwenye uume wako. Ili uwezo kufanikisha hatua hii ni lazima PORNOGRAPH iwekwe pembeni ilimsisimko USIO HALISI uliojengwa kutokana na picha hizo athari yake ianze kupungua kama siyo kutoweka kabisa.
Rewiring inamaanisha wakati ulipokuwa ukitazama filamu za ngono msisimko USIO HALISI wa ngono ulitengeneza njia mahususi, unapoacha kutazama picha hizo za uchi, njia hizo nazo hufifia na kupoteza athari yake. Ni sawa na kufanya mazoezi ya kunyanyua vyuma, unapoacha tu, baada ya muda kiuongo husika hurudi katika hali ya kawaida.
Njia za msisimko zilizo tengenezwa kwenye ubongo wako kupitia picha za uchi za kwenye mitandao zinapoanza kufifia kwa kuacha kutazama filamu hizo, njia HALISI na zilizo za kawaida kimaumbile zinaanza kujijenga na kufanya kazi yake kawaida na hapo uwezo wa jogoo wako kuwika mbele ya mtetea unaanza kurudi.
Kadiri siku zitakavyo anza kupita bila wewe kutazama filamu za uchi na ubongo wako ukijitibu taratibu, utaanza kuona mabadiliko kwenye mwili wako na hasa kwenye jogoo wako. Urijali utaanza kurudi, sasa mtetea anapo pita mbele yako, kwa ajili ya somo hili, tuseme upo ndani ya ndoa, mke wako akipita mbele yako utaanza kusisimka, na anapo vua nguo au kuonesha sehemu fulani za maumbile yake jogoo wako naye anaanza kushtuka, hongera ubongo wako umeanza kujitibu, na hatua hii ni ndani ya wiki tatu mpaka mwezi.
Muda utakavyo zidi kwenda ndivyo uwezo wako kwenye tendo la ndoa utakavyozidi kukua na utaanza kulifurahia tendo hilo na mke wako kuliko ulivyopata hapo kabla. Lakini si hivyo tu shughuli zako zingine za kijamii kiuchumi zitaanza kuwa na mwelekeo mpya, ilimradi kila kinacho kuzunguka kitaanza kutambua uwepo wako, thamani yako, mchango wako na ghafla utakuwa mtu mwingine kabisa.
Hata hivyo njia hii ya kuelekea kwenye matibabu haijanyooka, kama yalivyo maisha yetu njia hii nayo inayo uzito na wepesi katika safari ya kufikia hatua yakuwa huru kutokana na picha za uchi na kurudisha heshima ndani ya ndoa yako.
Kikwazo kikubwa ambacho utakutana nacho kwenye hatua hii ni kile ambacho anakutana nacho aina yeyote wa teja anapoamua kuanza safari ya kutoka kwenye shimo alilojichimbia mwenyewe. Hivyo basi kuna wakati utajikuta hitajio la kurudia kutazama picha za uchi kwenye mtandao ni kubwa mno, kiasi kwamba huwezi kufanya chochote au huwezi kujizuia kwamba lazima ufanye.
Hapo ndipo palipo na mtihani, hapo ndipo uwezo wako wa kufanya maamuzi na kuyasimamia unapokuwa kwenye majaribio, hapo ndipo unapoweza kupanda kuelekea kwenye safari yako ya kupona na kuiokoa ndoa yako, au kufuata matamanio yako na kurudi chini kuanza moja tena. Hivi ni vita na lazima uamue kushinda mara moja na mara moja basi.
Lakini haijalishi ni kiasi gani ulizama katika kaburi hilo la picha za uchi, unapoamua kuanza kutoka kwenye kaburi hilo, haijalishi ni mara ngapi utaanguka na kurudi chini, kuanza moja, kumbuka hakuna kukata tamaa, pambana kila nukta ya uhai wako kutoka kwenye kaburi hilo, na Inshallah siku moja utasimama kando ya kaburi hilo na kuanza kulifukia ili mwingine asije akatumbukia kama ilivyo tokea kwako.
Hivyo wakati umeshika kamba ya kukutoa kwenye kaburi hili, katika hatua za awali nguvu ya kukurudisha kwenye shimo la filamu za uchi zitakuwa kubwa kuliko nguvu za kutoka kwenye shimo hilo, lakini kadiri unapo piga hatua moja kuelekea nje ya shimo hilo, hata kama ukasogea kwa nchi moja, ujue hayo ni mafanikio, utambue siku hiyo umenyanyuka nchi moja kutoka kwenye shimo hilo, na siku moja utakuwa nje ya shimo hilo, na utakuwa huru, huru na mwenye nguvu na furaha, na hatimaye mke wako utafurahi kukuona Baba wa familia umerudi kwenye kiti chako kama baba, kuanzia chumbani mpaka kwenye majukumu mengine ya kifamilia hadhi yako itakuwa imerudi, na utajisikia furaha watoto wako wakikukimbilia na kusema BABA! BABA! Na mwenza wako akikusubiri kwenye kizingiti cha mlango kwa tabasamu pana sababu anajua kweli BABA wa nyumba amerudi na kila kitu kitakwenda sawa!
Kama ilivyo kwa teja wa aina yeyote yule, njia zilizo jengwa katika ubongo na kupelekea wewe kuwa ni teja wa kitu hicho na kwenye somo letu hapa ni teja wa picha za uchi, njia hizo kwenye ubongo hazifutiki hata kidogo, zitafifia tu na kuwa dhaifu, lakini daima zitakuwepo pale, hivyo ni kusema basi usijaribu tena hata kidogo kujaribu kulifukua kaburi hilo hata kwa sekunde moja! Punde tu unapogusa picha ya uchi kwenye mtandao wa picha za uchi ni kama kumuamsha chatu aliyelala, atakumeza tu na muda si muda utajikuta tena upo ndani ya kaburi hilo ukijiuliza umefikaje hapo.
Hapa ni baadhi tu ya maoni kutoka kwa watu ambao wamefanikiwa kusimama juu ya kaburi la picha za uchi na wanaelezea namna gani waliweza kufanya hivyo na wewe utaangalia kipi kitafaa kwako.
  1. Hakuna tena Porno.
  2. Hakuna fantasia za porno.
  3. Hakuna punyeto.
  4. Hakuna nyege mshindo (kwa muda wote wa zoezi hili)
  5. Kujichanganya na watu kwa wingi zaidi.
  6. Kufanya vitu mbadala na vitu vipya kama mazoezi na mengineyo yatakayo kuweka mbali na mitandao ya picha za uchi.
Njia bora ya kutoka kwenye shimo hilo ni kuupa ubongo wako muda wa kutosha wa mapumziko kutokana na kitu chochote kile kinacho husiana na ngono au punyeto. Ni muda gani wa mapumziko utajipatia, hii inatofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu ikichangiwa na umri, muda ambao ubongo wako umeathirika kutokana na picha hizo.
Udhaifu wetu mkubwa upo kwenye kukata tamaa. Njia ya uhakika kabisa ya kufanikiwa ni kujaribu tena na tena kila unapoanguka.
Kwa leo ni achie hapa … anza mchakamchaka wa kutoka kwenye shimo hilo, jipatie mwezi mmoja na utaiona dunia yako imebadilika … usisahau kuacha maoni yako hapo chini.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post