JPM AWATAKA WAKANDARASI NCHINI KUJITATHMINI

SHARE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Waziri Mkuu na Mjumbe wa Baraza hilo Kassim Majaliwa, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza Hilo kutoka Sekta Binafsi (TPSF) Dkt. Reginald Mengi, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji wa TBNC Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira, Vijana, Bunge na Watu wenyeulemavu Jenister Muhagama.
A
Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji wa TBNC Balozi John Kijazi akitoa utambulisho wa wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza hilo na uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
A 1`
 Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Baraza hilo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
A 2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Mwenyekiti Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF) Dkt. Reginald Mengi wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri Mkuu na Mjumbe wa Baraza hilo Kassim Majaliwa.
A 3
 Rais wa Taasisi ya Wakuu wa Makampuni CEO Round Table Ally Mfuruki akisalimiana na Mwenyetiki wa Taasisi za Kibenki ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage.
A 4
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Godfrey Simbeye akiteta jambo na Gavana wa Benki Kuu (BOT) Profesa Benno Ndulu wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
A 5
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakichangia mada wakati wa mkutano huo ulifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
A 6
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
A 7
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
A 8
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akielezea jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
A 9
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dkt. Reginald Mengi akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) Mhandisi Raymond Mbilinyi (katikati) na Mkurugenzi wa TPSF, Godfrey Simbeye.
A 10
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhandisi, Mussa Iyombe akielezea jambo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospether Muhongo (katikati), Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe (kushoto).
A 11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakati wa Mkutano wa 10 hilo uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Waziri Mkuu na Mjumbe wa Baraza hilo Kassim Majaliwa, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dkt. Reginald Mengi, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TBNC, Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira, Vijana, Bunge na Watu wenyeulemavu Jenister Muhagama.
……………………
Na Jacquiline Mrisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wakandarasi nchini kujitathmini, kurekebisha makosa yao pamoja na kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali badala ya kuilalamikia kuwa haiwasaidii.
Rais Magufuli ameyabainisha hayo wakati akiongea na wafanyabiashara wa sekta binafsi katika mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema kuwa tenda mbalimbali za ujenzi wa miundombinu zimekuwa zikitolewa na Serikali mara kwa mara lakini wakandarasi nchini wamekuwa hawazitumii fursa hizo na matokeo yake zinatolewa kwa wakandarasi kutoka nchi zingine.
“Serikali inatangaza tenda nyingi za ujenzi wa miundombinu na kwa kiasi kikubwa huwa inawalenga wakandarasi wa ndani kuliko wanaotoka nje lakini wakandarasi wetu wamekuwa hawazitumii fursa hizo, Serikali itachoka kuwabeba hivyo wakae wajitathmini,” alisema Rais Magufuli.
Ameongeza kuwa wakandarasi wanatakiwa kuungana na kufanya kazi kwa pamoja ili waweze kupata tenda zinazotolewa na Serikali kwa urahisi pia amewataka wawe wazalendo katika upangaji wa bei za kazi zao.
Akitoa mfano wa kukosa uzalendo, Rais Magufuli amesema kuwa wakandarasi wa hapa nchini walipoombwa kutoa bei za ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walitaja kiasi cha shilingi kati ya bilioni 150 na 200 wakati Wakala wa Majengo (TBA) waliyajenga kwa bilioni kumi tu.
Aidha, Rais Magufuli amewapongeza wafanyabiashara wa sekta binafsi kwa kushirikiana na Serikali katika kujenga uchumi wa viwanda na kuwahakikishia kuwa Serikali iko pamoja nao katika kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
Kwa upande wake Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa siku moja kwa taasisi zinazohusika na huduma za bandari zikiwemo za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuanza kutoa huduma zao kwa saa 24.
“Tumeamua kufanya hivyo ili kurahisisha huduma kwa wafanyabiashara kwani wamekua wakipata shida kwa kutumia muda mrefu kupata huduma katika bandari yetu, nafikiri njia hiyo itachochea wafanyabiashara kuwekeza zaidi”, alisema Mhe. Majaliwa
Ametoa rai kwa wafanyabiashara wa sekta binafsi kuwekeza kwenye kilimo kwani maendeleo ya ujenzi wa viwanda unategemea malighafi zinazotokana na kilimo.
Aidha Majaliwa alisema Serikali imekusudia kupanua wigo katika sekta ya kilimo kwa kuleta zana bora za kilimo, kuendelea kupunguza kodi katika mazao pamoja kuiwezesha Benki ya Kilimo kuendelea kutoa mikopo kwa wingi.
Nae, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Dkt. Reginald Mengi ameipongeza Serikali kwa kutekeleza ahadi mbalimbali walizojiwekea zikiwezo za elimu bure, ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa ndege pamoja na kukaa na wananchi na wadau mbalimbali kusikiliza na kutatua changamoto zao,
“Ushiriki wa wadau kwenye kikao hiki ni muendelezo chanya wa mahusiano mazuri kati ya Serikali na sekta binafsi, ninaamini majadiliano haya yatatatua changamoto za wafanyabiashara wa sekta binafsi”,alisema Dkt. Mengi.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: JPM AWATAKA WAKANDARASI NCHINI KUJITATHMINI
JPM AWATAKA WAKANDARASI NCHINI KUJITATHMINI
https://4.bp.blogspot.com/-9Uf7cvOcXlY/WQ41WYOs9vI/AAAAAAAAawI/cbUup44YXzMNa1FSqLiw0pzdTKgl0WOEwCLcB/s1600/unnamed-17.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-9Uf7cvOcXlY/WQ41WYOs9vI/AAAAAAAAawI/cbUup44YXzMNa1FSqLiw0pzdTKgl0WOEwCLcB/s72-c/unnamed-17.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/jpm-awataka-wakandarasi-nchini.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/jpm-awataka-wakandarasi-nchini.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy