JUVENTUS YAIFUNDISHA SOKA MONACO NA KUELEKEA KUTINGA FAINALI UEFA

Juventus inakaribia kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili katika misimu mitatu wakati Gonzalo Higuain akiifunga mara mbili Monaco katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali.

Wenyeji Monaco wakiwa nyumbani Ufaransa walianza vyema, huku mchezaji kijana Kylian Mbappe akimjaribu kipa Gianluigi Buffon kwa mpira wa kichwa na kisha baadaye akaokoa mchomo mwingine wa chini.

Lakini ilikuwa Higuain aliyetikiza nyavu akipata msaada wa Dani Alves na kunasa pasi ya kisigino ya Mbrazili huyo katika dakika ya 29, na kisha baadaye Higuain tena akaongeza goli la pili katika kipindi cha pili.
                                         Gonzalo Higuain akiachia shuti na kufunga goli la kwanza

                         Gonzalo Higuain akifunga goli la pili na kuifanya Monaco kutota nyumbani
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post