KADA WA CHADEMA AKAMATWA SAA TISA USIKU NYUMBANI KWAKE KIGAMBONI

Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Yericko Nyerere amekamatwa na watu wanaodhaniwa kuwa ama Askari Polisi au maofisa wa usalama wa taifa, usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa taarifa ya Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, Yericko alikamatwa majira ya saa tisa za usiku na watu waliofika nyumbani kwake wakiwa wamevalia kiraia.
Wakamataji hao waliokuwa wameongozana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbutu kilichopo Wilaya ya Kigamboni hawakueleza sababu za kijana huyo kukamatwa.
“Nimepata taarifa kutoka kwa ndugu wa Yericko ambao wamenipigia simu alfajiri leo. Wamesema amekamatwa saa tisa usiku na watu hao ambao walivalia kiraia. Viongozi wa Chadema wanaelekea polisi kufuatilia kwa kina chanzo cha Yeriko kukamatwa,” amesema Jacob
Hii si mara ya kwanza kwa kada huyo kukamatwa, kwani kipindi cha nyuma alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kimtandao.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post