KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL) YASITISHA SAFARI ZA TRENI

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitisha huduma ya usafari wa treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Bara kuanzia leo Mei 18, 2017 hadi itakapotangazwa tena.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kutokea uharibifu wa miundombinu ya reli leo asubuhi katika Stesheni za Ruvu na Ruvu Junction uliosababishwa na mvua kubwa zinazonyesha maeneo hayo ya Mkoa wa Pwani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya kusitisha huduma kwa muda, treni ya Deluxe iliyokuwa iondoke Dar es Salaam leo saa 2 asubuhi kwenda Kigoma imefutwa na abiria wametakiwa wafike stesheni kwa ajili ya kurejeshewa nauli zao.
Wakati huo huo uongozi wa TRL tayari umeelekea eneo la tukio ili kupanga mikakati ya haraka kukarabati miundombinu hukisa likiwemo daraja la Ruvu.
Aidha, uongozi umefafanua katika taarifa yake kuwa, katika kipindi cha mpito, treni ya abiria kutoka Mwanza na Kigoma itaishia Morogoro hadi njia ya Dar es Salaam na Morogoro itakapofunguliwa tena.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post