KAULI YA IGP SIMON SIRRO KUHUSU MAUAJI MKOANI PWANI

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro leo amezungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ikiwa ni mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari tangu alipoteuliwa na kuapishwa kushika wadhifa huo.
IGP Sirro amezungumzia mambo mengi lakini akijita zaidi katika masuala ya ulinzi na usalama wa raia, hasa mkoa wa Pwani ambapo mauaji ya raia yamekuwa yakitekelezwa na watu wasiojulikana.
Sirro amesema kuwa nchi kwa sasa iko shwari kwa sababu hakuna matukio makubwa yaliyoripotiwa isipokuwa katika Wilaya za Rufiji, Mkuranga na Kibiti mkoani Pwani ambapo matukio kadha wa kadha ya mauaji yamekuwa yakitokea.
Akizungumzia mauaji hayo yanayodaiwa ndiyo kilikuwa chanzo kikubwa cha Ernest Mangu kuondolewa madarakani, alisema kuwa hakuna kikundi chochote cha watu kilichopo juu ya sheria, na kuwa, mtu yeyote akitenda kosa ajue adhabu itamfuata.
Sirro amesisistiza kuwa suala la uhalifu mkoani Pwani ni la muda mfupi na kwamba, yeye na timu yake watalipatia majibu hivi karibuni. Aidha, Sirro amesema kuwa yeye mwenyewe kama IGP atatoa Tsh milioni 10 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wahusika wa matukio ya mauaji mkoani Pwani.
Kama alivyosema siku ya kuapishwa kwake, IGP Sirro amerudia leo kuwasihi wananchi watoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kutokomeza vitendo vya kihalifu, kwani pasi na ushirikiano, suala la kumaliza uhalifu litakuwa gumu. Sirro amesema kumekuwapo na madai ya Polisi kutumia nguvu kupita kiasi, na kusema atalifanyia kazi hilo ila lengo kubwa ni lazima wawashinde maadui.
Mbali na suala la mauaji mkoani Pwani, IGP Sirro alisema pia taarifa zinazoenezwa kwa amekuja na kikosi kipya cha Makamishna na Makamanda wa Polisi si za kweli na kwamba, watabaki wale wale waliokuwapo siku zote.
Aidha, Sirro alizungumzia suala la uhusiano wa raia na Polisi. Akianzia mkoani Pwani, aliwataka wote wanaojua kuwa ni raia wema na wamekimbia makazi yao, kurejea majumbani mwao. Lakini pia alisema, Polisi kiutaratibu haruhusiwi kumpiga mwandishi wa habari, na kama kuna yeyote aliyepigwa, watachunguza sakata hilo.
Sirro hakuishia kwa wananchi, lakini pia amewataka Askari Polisi kuacha mara moja tabia ya kuchukua rushwa huku akisema kuwa, ndani ya Jeshi hilo kuna utaratibu wa kuwaadhibi Askari wanaofanya vitendo hivyo, lakini pia wakuwapongeza wanaokataa na kuripoti vitendo vya rushwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post