KESI YA MUIGIZAJI WEMA SEPETU ‘YAIVA’ MAHAKAMANI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana iliambiwa kuwa upelelezi wa kesi ya muigizaji Wema Sepetu ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi umekamilika .
Taarifa hiyo ilitolewa na upande wa Jamhuri mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba ambapo walisema shauri hilo linaweza kusikilizwa sasa baada ya upelelezi kukamilika.
Hakimu Simba alisema kuwa, kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, maelezo ya wali ya kesi hiyo yatasikilizwa Juni Mosi mwaka huu na dhamana ya mtuhumiwa huyo itaendelea.
Katika Kesi ya msingi, Wema Sepetu anatuhumiwa kukutwa na msokoto mmoja wa bangi, na vipande viwili vya bangi vyenye uzito wa 1.08gramu.
Mbali na Sepetu, washtakiwa wengine ni wafanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa (21) na Matrida Abas (16) ambao wote wameunganishwa kwenye kesi hiyo ya msingi.
Washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post