KIJANA ANAYEFANANA NA MESSI AZUA TAHARUKI IRAN

Mwanafunzi mmoja nchini Iran anayeitwa Reza Parastesh anusurika kufungwa gerezani kwa kuwa amefanana sana na mchezaji wa klabu ya Barcelona Lionel Messi.
Watu wengi sana walikusanyika kutaka kupiga picha ‘selfie’ na Parastech katika mji wa Hamedan, kiasi ambacho polisi walimkamata na kumpeleka kituoni, ili kuepusha msongamano wa watu na vurugu zilizokuwapo eneo hilo.
 A woman poses for a selfie with the Lionel Messi lookalike on the streets of Tehran on May 8
Mfanano wake na mchezaji Messi ni mkubwa sana kiasi ambacho Eurosport UK walitumia picha yake wakiripoti habari za Messi.
Reza Parastesh, a doppelganger of Barcelona and Argentina's footballer Lionel Messi, walks down a street in Tehran on May 8
Habari za Parastesh zilianza kusambaa miezi kadhaa iliyopita baada ya baba yake ambaye ni shabiki mkubwa wa mpira wa miguu kumtaka kijana huyo mwenye miaka 25 kupiga picha katika mikao mbalimbali akiwa amevalia jezi ya Barcelona namba 10, kisha kuzituma katika mitandao ya michezo.
“Nilizituma picha hizo jioni na asubuhi yake nilipokea simu ikinitaka niende kwa ajili ya mahojiano” aliiambia AFP.
Kwa sasa kijana huyo amekuwa akiitwa kwa ajili ya mahojiano na vituo balimbali vya habari na kampuni za mitindo zimeanza kutaka kufanya kazi na yeye.
“Kwa sasa watu wananiona kama Messi wa Iran, na wanataka niige kila kitu anachokifanya Messi. Kila nikitokea mitaani watu wanashangazwa sana na muonekano wangu” alisema Parastesh.
The student was reluctant at first, but eventually grew into the role, wearing the Barcelona strip out in public, growing his hair and beard to match the footballer and carrying a ball
Watu wa Iran wanafurahishwa sana na mpira wa miguu, na Parastesh anajikuta akikabiliwa mara kwa mara na watu wakitaka kupiga naye picha ‘selfie’.
“Ninafurahishwa kuona watu wanafurahia uwepo wangu. Hii inanipa nguvu na kunitia moyo,” aliongeza.
Parastesh anapenda mpira sana japo hajawahi kuucheza kama fani yake. Kwa sasa anajifunza namna mbalimbali za kuuchezea mpira ili aweze kuigiza uhalisia wa Messi.
Reza Parastesh, a doppelganger of Barcelona and Argentina's footballer Lionel Messi, walks down a street in Tehran on May 8
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post