KIONGOZI WA NGAZI YA JUU WA SIMBA AJIUZULU SABABU YA SAKATA LA MO DEWJI

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba ameamua kujitoa kwenye uongozi klabu hiyo kuepuka kuwa sehemu ya watu wasio waungwana.
Akizungumza jana Hans Poppe amesema, uongozi wa Simba chini ya Rais Evans Elieza Aveva umemfanyia mambo yasiyo ya kiungwana kwa mwanachama Mohammed ‘Mo’ Dewji.
Hans Poppe amejiuzulu Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba na maana yake amejivua pia na uongozi wa Kamati ya Usajili na ya ujenzi wa Bunju Complex baada ya kuchukizwa na kutohusishwa katika mkataba wa udhamini wa kampuni ya SportPesa.
Zacharia Hans Poppe (kulia) amesema hataki kuwa sehemu ya watu wasio waungwana Simba
“Siyo kushirikishwa mimi tu, bali Wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji pia, lakini kubwa zaidi tuna makubaliano na Mo (Dewji) kuwa tukitaka kuingia mkataba na yeyote Yule, hakatai lakini tumshirikishe, sasa tunasaini mkataba kwa kumzunguka ni kukosa uungwana na siwezi kuwa sehemu ya hilo,”amesema.
Poppe amesema kwamba alijaribu sana kutaka kukutana na viongozi wa Simba kujadili nao suala hilo, lakini walikuwa wanamkwepa ndiyo maana ameamua kujiuzulu; “Hatujakaa, kila nikiwaambia tulijadili wanaingilia huku wanatokea kule,”.
Dewji anayetaka kununua hisa Simba, amesikitishwa na uongozi wa klabu hiyo kwa kuingia mkataba wa udhamini na kampuni ya SportPesa bila kumshirikisha.
Na habari ambazo hazijathibitishwa na upande wowote, zinasema Mo Dewji, Mbunge wa zamani wa Singida Mjini ameuandikia barua uongozi wa klabu hiyo chini ya Rais wake, Evans Aveva kudai alipwe fedha zake, Sh Bilioni 1.4 alizokuwa anaikopesha Simba kwa kulipa mishahara ya wachezaji na benchi la Ufundi, Sh Milioni 80 kila mwezi.
Imedaiwa Mo Dewji alikuwa anatoa fedha hizo kwa makubaliano zitalipwa wakati mpango wake wa kununua hisa za klabu utakapokamilika. Mo alikubaliana na uongozi wa Simba kununua asilimia 51 ya hisa kwa Sh. Bilioni 20 mara baada ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba utakapokamilika.
Lakini zoezi hilo linaelekea kuingia doa baada ya Mo Dewji kuandika katika ukurasa wake wa Twitter akilalamikia uongozi wa klabu kuingia mkataba na SportPesa bila kumshirikisha.
Na upande mwingine, uongozi wa Simba na umemeguka baada ya Hans Poppe naye kuandika barua ya kujiuzulu, naye pia akilalamikia kutoshirikishwa katika mkataba wa SportPesa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post