KUHUSU KAMBI YA MISRI, SAMATTA AOMBA RUHUSA TAIFA STARS, KUKUTANA NA WENZAKE DAR

Msafara wa kikosi cha wachezaji 20 wa Taifa Stars kinachodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti, kinatarajiwa kuondoka Jumanne hii saa 10.45 jioni kwenda Misri.
Taifa Stars inakwenda Misri kufanya kambi ya siku nane kujindaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao 20 kutoka hapa Tanzania wataungana na na wengine watatu, nahodha Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Faridi Mussa wanaocheza ughaibuni katika kikosi hicho na kufanya jumla ya wachezaji kuwa 23.
Lakini taarifa kutoka ndani ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) zinaeleza kuwa Samatta ameomba ruhusa ili ajiunge na timu itaporejea jijini Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametaja kikosi kitakachosafiri kwenda kambini kujiandaa na mchezo huo wa Kundi L kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon.

Kikosi cha Taifa Stars kinaundwa na:

Makipa;
Aishi Manula (Azam FC), Benno Kakolanya (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

Walinzi;
Shomari Kapombe (Azam FC), Hassan Kessy (Yanga SC), Mohammed Hussein (Simba), Haji Mwinyi  (Yanga SC), Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Agrey Morris (Azam FC).

Viungo;
Himid Mao (Azam FC), Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Mzamiru Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga SC), Shizza Kichuya (Simba SC) na Farid Mussa (Teneriffe, Hispania).

Washambuliaji; 
Mbwana Samatta (KRC Genk - Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna - Sweden), Ibrahim Ajibu (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting).

Wasaidizi wa Mayanga katika benchi la ufundi ni Novatus Fulgence ambaye ni kocha msaidizi Patrick Mwangata - kocha wa makipa pia yumo Meneja wa timu, Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu, Daktari wa timu ni Richard Yomba na Daktari wa viungo ni Gilbert Kigadya.
Timu hiyo iliingia kambini Machi 23, 2017 kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam kabla ya kesho kwenda Misri na baadaye itarejea Tanzania kucheza na Lesotho, Juni 10, mwaka.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post