LINAH APATA DILI LA DIAMOND

Maduka makubwa ya nguo za watoto yamekuwa utaratibu wa kujitangaza kupitia watoto wa wasanii na watu maarufu, kama ambavyo watoto wa Diamond wanavyotumiwa kuwa mabalozi wa baadhi ya maduka hayo.
Msanii wa muziki wa Bongo fleva, Linah Sanga anayetarajia kupata mtoto hivi karibuni amepata dili ambapo mtoto atakayezaliwa atakuwa balozi wa duka la nguo za watoto la a Kids City Shopping (KCS).
Linah ambaye mapema wiki hii alitambulisha herufi ya mwanzo ya jina la mtoto anayemtarajia baada ya kuweka picha ya ujauzito kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika ‘Baby T on the way’,anakuwa miongoni mwa mastaa ambao watoto wao wamepata bahati ya kuwa mabalozi.

“Kwa mara ya kwanza nitazungumza na mashabiki wangu mwishoni mwa wiki hii kwa niaba ya KCS ambao ni wauzaji wa bidhaa mbalimbali za watoto na akinamama wajawazito,” amesema Linah.
Mwanadada huyo ambaye hivi karibuni alimtangaza mpenzi wake anayetarajia kuwa baba wa mtoto wake aitwaye Shabani ambaye pia ni bosi wake, Linah amedai kuwa anafuraha kuwa mjamzito kwa kuwa ni kitu ambacho alikuwa akitamani kwa muda mrefu.
Mzazi mwenzake ambaye pia ni mkurugenzi wa Kampuni Drops Up Entertainment ambayo inamsimamia Linah, amesema wamejipanga kuhakikisha Linah anafika mbali zaidi kimziki.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post