MAALIM SEIF AELEZA SABABU MOJA ILIYOPELEKEA KUTOPOKEA MKONO WA DK. SHEIN

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif  Sharrif Hamad leo katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa katika runing ya Clouds ameeleza  jambo lililomfanya akatae kupokea mkono wa salamu kutoka kwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein.
Akizungumza katika kipindi hicho, Maali Seif alisema kwamba, kukataa kwake kupokea mkono wa salamu kutoka kwa Dk. Shein ilikuwa ni ishara ya kupeleka ujumbe kuwa alikasirishwa na kitendo cha yeye kuporwa haki yake.
Maalim Seif aliyekuwa mgombea wa urais Zanzibar kwa tiketi ya CUF mwaka 2015, alitangaza kuwa yeye ndio mshindi kinyume na utaratibu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), jambo lililopelekea Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jecha Salum Jecha kufuta uchaguzi na kuutaka urudiwe upya.
Tukio la Maalim Seif kukataa mkono wa Dk. Shein ni katika mazishi ya aliyekuwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi.
Alisema kuwa alikasirishwa na kitendo cha yeye kuporwa haki yake na Tume ya Uchaguzi iliyokuwa chini ya uongozi wa Jecha.
“Nilifanya makusudi kutompa mkono Rais Shein ili apate ujumbe kuwa nilikasirika kuporwa haki yangu” alisema Maalim Seif
Aliongeza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Salum Jecha hakushirikisha wenzake katika kutoa maamuzi ya kuufuta uchaguzi huo bali alitumia ubabe.
“Jecha alifuta uchaguzi kwa ubabe bila kushirikisha wenzake sababu hata katiba ya Zanzibar haimpi mamlaka ya kufuta uchaguzi” alisema.
Alipoulizwa kuhusu suala la mgawanyiko uliopo sasa katika chama chake cha CUF, Maalim Seif alisema kuwa mgawanyiko huo ni mawazo ya watu pekee lakini CUF ni moja.
“Hakuna CUF ya Lipumba au CUF ya Maalim Seif, maamuzi yote ya chama yanafanywa na Baraza Kuu la chama” aliongeza.
Mgawanyiko huo umekuja baada ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba kujiondoa katika chama wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na baadae kurudi akidai kuwa yeye bado ni mwenyekiti halali wa chama hicho, hivyo kufanya kuwepo kwa makundi mawili ndani ya chama hicho, moja likimuunga mkono Maalim Seif na lingine likimuunga mkono Prof. Lipumba.
Hata hivyo Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini bado anamtambua Prof. Lipumba kama Mwenyekiri wa CUF na Maalim Seif kama Katibu mkuu wa chama hicho.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post