MAAMUZI YA KAMATI YA BUNGE BAADA YA KUWAHOJI HALIMA MDEE NA FREEMAN MBOWE

Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge la Tanzania, leo imewasilisha bungeni taarifa za matukio mbalimbali ambazo imezifanyika kazi ikiwa ni pamoja na kuwaita na kuwahoji wahusika kwa kukiuka kanuni za bunge nje na ndani ya bunge hilo.
Taarifa zilizowasilishwa na kamati hiyo ni pamoja na ile ya kudhara Mamlaka ya Spika wa Bunge, kosa lililofanywa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.
Taarifa nyingine ni ile ya kuingilia uhuru wa bunge kosa lililofanywa na Paul Christian Makonda na Alexander Mnyeti. Pamoja na hiyo, taarifa ya kudharau mamlaka ya spika wa bunge, kosa la Esther Bulaya pili iliwasilishwa leo bungeni.
Kufuatia taarifa hizo, maamuzi mbalimbali yametolewa ambapo, Mbunge Halima James Mdee amefungiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyosalia kwa kosa la kudharau Mamlaka ya Spika wa Bunge. kamati imesema kuwa Mdee amzuiwa kuhudhuria vikao vilivyosalia kutokana na kurudia makosa yake. Kwa upande wake Freeman Mbowe, kamati imemsamehe baada ya kukiri kutendo kosa hilo, Apili 4, mwaka huu.
Kwa upande wake Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya, amepewa na karipio kali kufuatia kudhaharau mamlaka ya soika wa bunge la Tanzania.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post