MADUDU YABAINIKA KATIKA VITABU VYA SHULE YA MSINGI

SHARE:

Wabunge washauri kuzuiwa matumizi ya vitabu vya kujifunzia vyenye makosa ili kuepuka kuendelea kuwaharibu wanafunzi shuleni. Makosa yaliy...

Wabunge washauri kuzuiwa matumizi ya vitabu vya kujifunzia vyenye makosa ili kuepuka kuendelea kuwaharibu wanafunzi shuleni. Makosa yaliyobainika katika vitabu hivyo ni ya kisarufi, mpangilio wa kurasa, tafsiri sisisi na kimantiki.
Wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2017/18 bungeni mjini Dodoma jana kwa nyakati tofauti tofauti, walisema vitabu hivyo vina makosa mengi ya lugha ya Kiswahili na Kingereza jambo ambalo linaua elimu nchini
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Suzan Lyimo alipokuwa anasoma maoni ya kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, alisema pia makosa hayo yamekithiri katika herufi kubwa na ndogo na matumizi ya nukta pacha.
“Matatizo hayo yamo kwenye vitabu vyote hasa kujifunza kusoma, kuandika, kuhesabu, afya na mazingira, michezo na sanaa,” alisema.
Alitoa mfano wa Kitabu cha Najifunza Kusoma, darasa la Kwanza, ukurasa wa 99 kinataja kucha kikimaanisha ukucha. Pia kitabu hicho kinaeleza kumjulisha bila kubadili kwa wima (baada ya kumjumulisha kwa wima bila kubadili) ukurasa 93 na 94 maneno chupa/ chupa ya chai (yakichanganywa)
Lyimo alisema kitabu cha I Learn English Language, kina matatizo ya matumizi ya herufi kubwa na ndogo mengi mno karibuni kila ukurasa
“Inaelekea pia mwandishi hana uwezo wa kutosha wa lugha yenyewe kwani kuna makosa mengi.”
Alitoa mfano wa sentensi ambazo zimekosewa kuwa ni These are my parent, which is long between a pen and ruler? The driver is taken the police station, a boy is on bed at hospital na which is the big city of Tanzania (meaning Capital City).
“Vitabu vya darasa la kwanza vilichelewa kuchapishwa na kuwasilishwa shuleni. Hata hivyo, baada ya hekaheka nyingi za kuchoma nakala zilizokuwa na makosa ya mchapishaji, baadhi ya vitabu vya darasa la kwanza vilitoka Juni, 2016 na baadhi ya Januari mwaka 2017,” alisema.
“Kwa hali hiyo ya utoaji wa vitabu vipya na ucheleweshaji, walimu na wanafunzi watapata shida kubwa kuutumia mtaala mpya,” aliongeza
Lyimo aliitaka Serikali kuzuia matumizi ya vitabu hivyo vyenye makosa shuleni na pia kuiagiza taasisi elimu kufanya marekebisho ya makosa yaliyopo kwenye vitabu hivyo na kuvichapisha upya.
Aidha, aliitaka Serikali kufanya uhakiki wa taaluma na weledi wa watumishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania ili kujiridhisha kama wana sifa stahiki, uwezo na weledi katika kufanya kazi utunzi wa vitabu
Awali, katika hotuba yake ya bajeti Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema, “Uchambuzi wa kina unafanyika kwa vitabu vyote vilivyochapishwa mwaka 2016/17 ili kubaini endapo kuna dosari zilizobainika…”
Alisema mchakato wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za utumishi umekwishaanza kwa watumishi ambao vitabu walivyoidhinisha vimebainika kuwa na makosa.
“Napenda kulihakikishia Bunge lako tukufu kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika ili kukomesha tabia ya uzembe kwenye kazi muhimu za Taifa,” alisema.
Alisema baada ya uchambuzi wa vitabu vyote vilivyochapwa kukamilika, wizara itaamua hatua za kuchukua dhidi ya vile ambavyo vitabainika kuwa na dosari
“Nawahakikishia wabunge kuwa wazembe wote waliokuwa sio makini katika hili kuangalia vitabu hivi tutawaadhibu. Nawahakikishia tutasafisha taasisi hii (Taasisi ya Elimu Tanzania ­ TIE),” alisema.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MADUDU YABAINIKA KATIKA VITABU VYA SHULE YA MSINGI
MADUDU YABAINIKA KATIKA VITABU VYA SHULE YA MSINGI
https://4.bp.blogspot.com/-Ju7XaPeuVrU/WRhBYWxvoGI/AAAAAAAAbMQ/c0Qrtul1Bj0xsUzcDCB-MvIIiLjkFlKPQCLcB/s1600/picwabunge.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-Ju7XaPeuVrU/WRhBYWxvoGI/AAAAAAAAbMQ/c0Qrtul1Bj0xsUzcDCB-MvIIiLjkFlKPQCLcB/s72-c/picwabunge.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/madudu-yabainika-katika-vitabu-vya.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/madudu-yabainika-katika-vitabu-vya.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy