MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR, BALOZI SEIF AONGOZA MAADHIMISHO YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

SHARE:

Balozi Seif Ali Iddi kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Habari Nchini...

Balozi Seif Ali Iddi kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Habari Nchini mara baada ya kufungua mdahalo wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga, kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Mitawi. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema haja ya vyombo vya Habari kujitathmini hivi sasa ni kubwa zaidi kuliko wakati mwengine wowote ule katika Historia ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa vile vinapita katika kipindi kigumu cha kutokuaminiwa na Wananchi.

Alisema dhana ya Habari isiyoaminika ambayo kwa sasa imeanza kutumiwa na baadhi ya Viongozi wakubwa Duniani inaitafuna kada ya uandishi wa Habari na kupelekea Watu kutilia mashaka Habari zinazotolewa na vyombo vya Habari.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani hapo katika Ukumbi wa Chuo cha Habari Zanzibar kiliopo Kilimani Mjini Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema maafa ya kuporomoka kwa Uandishi wa Habari kwa kutokuaminiwa na Jamii ni janga kubwa kuliko maafa Yanayoweza kuletwa na Mama wa Mabomu yote.

Balozi Seif alisema Uandishi wa Habari Makini ni ule unaofuata na kuzingatia Maadili kwa kutumia Utafiti wa kutosha kabla ya kuchapisha au kuzitangaza Habari na pale makosa yanapotokezea kwa bahati mbaya Wana Habari wanakuwa waungwana kwa kuyarekebisha mara moja.

Alielezea matumaini yake kwamba pale baadhi ya Wanahabari watakapoamua kurejea kwenye misingi yao ya kazi kwa kujitenga na Propaganda, upendeleo, ushabiki wa Kisiasa na kusimama kwenye ukweli mtupu imani ya Walimwengu kwa Vyombo vya Habari itarejea kama kawaida.

Balozi Seif alitoa changamoto kwa Waandishi wa Habari Nchini kulitafutia ufumbuzi wa kudumu tatizo linalokera la upotoshaji wa Habari linalofanywa na baadhi ya Waandishi hasa wakizingatia wazi kwamba mchango wa Vyombo vya Habari kwa maendeleo ya Taifa hauna mfano wake.

Aliwataka Wanahabari wazingatie maneno aliyoyasema Mwandishi wa Habari Mkongwe wa Gazeti la New York Times la Marekani Bwana Jim Rutenberg pale aliposema “ It will be great Journalism that saves Journalism” kwa tafsiri isiyo rasmi:- Uandishi wa Habari makini ndio unaookoa uandishi wa Habari.

Akizungumzia Uhuru wa Vyombo vya Habari Nchini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwatoa wasi wasi Wanahabari kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuulinda Uhuru huo na endapo kama zipo sheria zinazokwamisha Uhuru wa Habari Serikali kupitia Wizara inayosimamia Sekta ya Habari itazifanyia marekebisho.

Balozi Seif alisema lengo la Serikali kuu ni kupanua zaidi Uhuru huo wa Vyombo vya Habari ambao ndio njia pekee itakayouhakikishia Umma utekelezaji wa dhana ya Utawala Bora ambao msingi wake ni Demokrasia, Uwajibikaji, Utawala wa Sheria pamoja na Uwazi.

Alisema Uhuru wa Habari husaidia kujenga Utamaduni wa kuheshimu Utawala wa sheria katika Nchi na wale watakaokwenda kinyume na kujiweka juu ya sheria ikiwa Viongozi au Watu wa kawaida Vyombo vya Habari vilivyo Huru havitosita kuibua udhaifu huo.

Balozi Seif alieleza kwamba ufichuaji wa maovu ndani ya jamii kama rushwa, Watu wanaojishughulisha na biashara ya Dawa za kulevya, wale wanaoendeleza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wakiwemo pia Viongozi wanaotumia vibaya madarakayao Serikalini utapatikana iwapo utakuwepo uhuru wa kutosha wa Vyombo vya Habari.

“ Serikali haina sababu ya kuogopa uwepo wa Uhuru wa Vyombo vya Habari Nchini kwa vile Uhuru huo ukitumiwa vyema utaleta faida kubwa zaidi kwa Taifa”. Alisema Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza umuhimu wa kuimarisha vyombo vya Habari ambavyo ni muhimili unaoweza kuwaunganisha au kuwatenganisha Wana Jamii kutegemea matumizi ya vyombo hivyo.Balozi Seif Ali Iddi aliwakumbusha Wanahabari kuendelea kuithamini Siku ya Uhuru wa Habari Duniani iliyotangazwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Mwaka 1993 na kuamuliwa kuadhimishwa Duniani kote kila ifikapo Tarehe 3 Mei ya kila mwaka.

Mapema Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar Omar alisema umakini wake wa kuwaandalia mazingira bora wana Taaluma wa Sekta ya Habari walioamua kujifunza Tasnia hiyo. 

Nd. Chande alisema ujenzi wa majengo mapya ya Chuo cha Habari Zanzibar umeleta faraja kubwa kwa Wanahabari wachanga ambao kwa kipindi kirefu walikuwa watu wa kuhama hama sehemu mojna hadi nyengine jambo ambalo lilikuwa likiwakosesha utulivu wa kujifunza.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Chuo cha Habari Zanzibar alisema Serikali bado ina jukumu la kuendelea kuunga mkono Tasnia hiyo kwa kuwapatia vifaa vinavyowasaidia kwenda na wakati wa mazingira ya sasa.

Akigusia suala la amani ambalo limo katika ujumbe wa mwaka huu wa siku ya Uhuru wa Habari Duniani Mkuu huyo wa chuo cha Habari Zanzibar alisema Mataifa yoyote Duniani yanaweza kukosa Amani iwao jamii zao zitakosa utulivu wa maisha.

Nd. Chande alisema kero mbali mbali zinazozikabili jamii ikiwemo migogoro ya Ardhi, ukosefu wa Bara bara na huduma za Maji safi na salama ni miongoni mwa machimbuko ya ukosefu wa Amani na hatimae dalili ya uwezo wa vita vya wenyewe kwa wenye huonekana.

Akitoa salamu za Baraza la Habari Tanzania {MCT} Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bwana Kajubi Mukajanga alisema Sera ya Baraza hilo ni kuona shughuli za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani zinafanyika sambamba Tanzania Bara na Zanzibar.

Bwana Kajubi alisema hatua hiyo itawapa fursa wanahabari kutafakari kwa kina muelekeo wa Sekta yao sambamba na kuzitafutia ufumbuzi changamoto wanazopambana nazo kila siku katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katibu Mtendaji huyo wa Baraza la Habari Tanzania amewashukuru washirika wa Habari Zanzibar ikiwemo chama cha Waandishi wa Habari wanawake {TAMWA}, Clabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar { Press Club } pamoja na Chuo cha Habari Zanzibar kwa ushiriki wao wa kufanikisha maadhimisho hayo ya siku ya Uhuru wa Habari Duniani.

Akimkaribisha mgeni rasmi katika Kilele cha Maadhimisho hayo ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud alisema siku hii ni muhimu kutokana na ushiriki wa pamoja kati ya Wanahabari, Wadau na Wananchi mbali mbali.

Mh. Ayoub alisema Mikutano ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Habari licha ya kuwapa fursa Wanahabari kutafakari mambo mbali mbali yanayojiri katika maeneo yao ya kazi lakini pia ushiriki wa wadau wengine hutoa nafasi ya kuzungumzia namna ya kukabiliana na changamoto zinazoisumbhua Tasnia hiyo ya Habari.

Mkuu huyo wa Mkoa Mjini Magharibi alivipongeza vyombo vyote vya Habari Nchini kwa umahiri wao wa kuendelea kushirikiana na Serikali katika harakati za kuwapasha Habari Wananchi juu ya Maendeleo mbali mbali yanayotekelezwa na Viongozi wa Serikali.

Mh. Ayoub alisema Mkoa Mjini Magharibi unajivunia uwepo wa vyombo vya Habari zaidi ya Asilimia 80% ndani ya Mkoa huo licha ya kuwepo malamiko ya baadhi ya Viongozi na Wananchi wa Mikoa mengine kusahauliwa katika matukio yanayoripotiwa kwenye vyombo hivyo.

Ujumbe wa Mwaka huu wa Siku ya Uhuru wa Habari Duniani unasema Critical mind for critical times:- the media’s role in advancing, peaceful, just and inclucive societies:- kwa tafsiri isiyo rasmi:- “ umakini wa fikra kwa wakati muhimu, nafasi ya vyombo vya Habari katika kuimarisha jamii yenye amani, haki na ujumuishwaji ”.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
3/5/2017.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR, BALOZI SEIF AONGOZA MAADHIMISHO YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR, BALOZI SEIF AONGOZA MAADHIMISHO YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
https://4.bp.blogspot.com/-fDOQoQ1ugVA/WQppdaEe9TI/AAAAAAAAae8/JIMZ3bJJSns-IyHCcX2Yql0370BJIl8fwCLcB/s1600/657.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-fDOQoQ1ugVA/WQppdaEe9TI/AAAAAAAAae8/JIMZ3bJJSns-IyHCcX2Yql0370BJIl8fwCLcB/s72-c/657.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/makamu-wa-pili-wa-rais-zanzibar-balozi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/makamu-wa-pili-wa-rais-zanzibar-balozi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy