MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI MAALUM YA MIMI NA WEWE

SHARE:

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkoa wa Mjini Magharibi,...

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar za kusaidia wananchi wanaokabiliwa na hali duni ya maisha kwa kuahidi kutoa mifuko ya saruji 1000 na mabati 600 kwa ajili ya kusaidia wananchi hao.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi hiyo mjini Unguja wakati anazindua kampeni maalum ya MIMI NA WEWE inayolenga kuhamasisha wananchi kuungana pamoja katika kutoa misaada ya hali na mali ili kuboresha huduma za kijamii katika sekta za afya, elimu,mazingira,maji safi na salama, matumizi bora ya ardhi na kusaidia watu wasiojiweza.
Makamu wa Rais katika hotuba yake kwa mamia ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hiyo amekemea vikali tabia ya ubinafsi kwa baadhi ya viongozi inayosababisha wananchi kutopatiwa taarifa muhimu za maendeleo yao hali inayopelekea uduni katika uchangiaji wa shughuli za maendeleo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ni muhimu kwa viongozi katika maeneo mbalimbali kujenga tabia ya kuweka wazi mapato na matumizi ya fedha wanazopata na jinsi zilivyotumika ili kuwapa moyo wananchi katika kuchangia kwenye shughuli za maendeleo kwa sababu watakuwa na imani kuwa fedha zao walizochanga zinatumika vizuri.
“Maendeleo endelevu ni lazima yazingatie Utu na heshima ya mtu, mshikamano wa dhati na mafungamano ya Kijamii,” Amesisitiza Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais pia amehimiza wadau mbalimbali wa maendeleo hasa sekta binafsi na wananchi kwa ujumla kujenga moyo wa kujitolea na kutoa misaada ili kuhakikisha taifa linasonga mbele kimaendeleo kuliko kutegemea wafadhili wa nje ya nchi tu.
Ameeleza kuwa kampeni ya Mimi na Wewe ina umuhimu wa kipekee kwani inakusudia kuwaomba na kuwahamasisha wananchi hasa wa Zanzibar kuchangia kwa hali na mali katika kusaidia wananchi wenzao ambao hali zao za maisha bado ni duni ili kutimiza malengo ya mapinduzi kujenga maisha bora na usawa kwa kila mtu.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuweka kando itikadi zao za kisiasa hasa wa Zanzibar na wajenge Zanzibar imara yenye upendo, umoja na mshikamano ili kuharakisha juhudi za maendeleo.
Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud amesema wameamua kuanzisha kampeni hiyo maalum ili kurejesha moyo wa kusaidiana miongoni wa Wazanzibar hatua ambayo itasaidia maradufu uboreshaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.
Mkuu huyo wa mkoa wa Mjini Magharibi amesema mkoa huo ndio unaongoza kwa kuwa na wananchi wengi kwa Zanzibar ambao wanafikia zaidi ya laki Tano hivyo idadi hiyo kubwa ya watu inahitaji rasilimali nyingi kwa ajili ya kuhudumia wananchi hao kitu ambacho bado ni changamoto kubwa inayohitaji ushirikiano ili kuipatia ufumbuzi.
Amesema anaimani kubwa kuwa kampeni maalum ya Mimi na Wewe itawaibua wadau wa maendeleo na wananchi wenyewe katika kutoa misaada mbalimbali ikiwemo kujitolea katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo jambo ambalo litasaidia kubadili maisha ya wananchi maskini kwa kuwasaidia kupata kipato kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Unguja- Zanzibar
22-May-2017.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI MAALUM YA MIMI NA WEWE
MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI MAALUM YA MIMI NA WEWE
https://4.bp.blogspot.com/-Fyfx5DMfp50/WSPMVwW6ZFI/AAAAAAAAbtM/ZaPmitrLf10NnU14nJPp1yls7ibqOEojwCLcB/s1600/3-702x375.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-Fyfx5DMfp50/WSPMVwW6ZFI/AAAAAAAAbtM/ZaPmitrLf10NnU14nJPp1yls7ibqOEojwCLcB/s72-c/3-702x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/makamu-wa-rais-azindua-kampeni-maalum.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/makamu-wa-rais-azindua-kampeni-maalum.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy