MAKONDA AKUTWA NA KOSA LA KUINGILIA UHURU WA BUNGE

Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge la Tanzania, leo imewasilisha bungeni taarifa za matukio mbalimbali ambazo imezifanyika kazi ikiwa ni pamoja na kuwaita na kuwahoji wahusika kwa kukiuka kanuni za bunge nje na ndani ya bunge hilo.
Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ile ya kuingilia uhuru wa bunge kosa lililofanywa na Paul Christian Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka bungeni, viongozi hao wate wawili wamesamehewa kutokana na kukiri makosa yao na kuliomba radhi bunge la Tanzania.
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imeazimia kumsamehe DC Alexander Mnyeti kutokana na kukiri na kujutia kosa lake na kuliomba radhi Bunge. Lakini pia, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imeazimia kumsamehe Paul Makonda kutokana na kukiri na kujutia kosa lake na kuliomba radhi Bunge.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post