MAMA ASIMULIA KAULI YA MWISHO YA MWANAE KABLA YA KUFARIKI KWENYE AJALI KARATU

Mmoja wa wazazi waliopoteza watoto wake katika ajali ya basi Wilayani Karatu, Arusha alisema kuwa mwanae, Rachel Gideon alimwambia usiku wa kuamkia jana kuwa atakwenda kufanya mtihani wa ujirani mwema wilayani Karatu.
Mama huyo, Esther Nelson aliyazungumza hayo alipokuwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru alipofika kutambua kama mwanae alikuwa miongoni mwa 33 waliofariki.
“Mwanangu aliniaga jana asubuhi alisema wanakwenda kufanya mtihani Karatu, sijui nitafanya nini mimi,”alisema mama huyo huku akilia kwa uchungu mkubwa.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa tatu asubuhi ambapo wanafunzi 33, walimu 2 wa Shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha, pamoja na dereva mmoja walipoteza maisha. Wanafunzi hao walikuwa wanakwenda katika katika shule ya mchepuo ya kiingereza, Tumaini Junior Academy ambapo walikuwa wanakwenda kufanya mtihani wa ujirani mwema.
Watu mbalimbali, taasisi za serikali na binafsi zimegushwa na msiba huo mkubwa uliolitikisa taifa, huku wakituma salamu za rambirambi kuwafariji familia, wakazi wa Arusha na watanzania kwa ujumla kutokana na janga la Taifa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post