MAMA SALMA KIKWETE AGEUKA ‘MBOGO’ BUNGENI

Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Salma Rashid Kikwete jana aligeuka mbogo bungeni wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi ya Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2017/18.
Mbunge Salma Kikwete akichangia hotuba hiyo bungeni jana, alipinga hoja ya watoto wa kike kuruhusiwa kurejea shuleni kuendelea na masomo baada ya kujifungua, huku akiitaka serikali kutafuta njia mbadala ya kuwasaidia watoto hao kupata elimu.
Salma Kikwete alisema uamuzi wa kuwaruhusu watoto hao kuendelea na masomo hautakuwa sahihi kutokana na mila, desturi, dini na mazingira ya kitanzania.
Mbali na Salma Kikwete kuipinga hoja hiyo, Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy alisema kuwa anaunga mkono hoja ya wanafunzi kutokuruhusiwa kuendelea na masomo wakipata ujauzito, huku akiwataka wabunge ambao walianza kufanya mapenzi wakiwa shuleni kutoa ushuhuda kama waliendelea kufanya vizuri kwenye masomo.
Mbali na baadhi ya wabunge kumuunga mkono, wengine hasa wa upinzani hawakuridhishwa na hoja aliyoitoa wakitaka wanafunzi hao kuruhusiwa kuendelea na masomo.
Mbunge wa Ndanda (CHADEMA), Cecil Mwambe alisema, Lindi na Mtwara ni miongoni mwa mikoa iliyoathirika zaidi na tatizo hilo, huku akimtaka Salma Kikwete ambaye naye anatokea Lindi kueleza sababu zaidi kwanini wanafunzi hao wasiruhusiwe kurejea shuleni kwa vile tu wamepata mimba.
Awali serikali ilikuwa imeahidi kuwa ingepeleka mwingozo bungeni kuhusu suala la wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni, lakini hadi sasa haijafanya hivyo.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post