MAMBO 11 ANAYOYATAKA MUME KUTOKA KWA MKE

Kuna mambo ambayo mwanaume huyataka kutoka kwa mwanamke lakini hayaweki wazi au kumwambia mkewe amfanyie.                        

Lengo langu sio kudadisi sababu zinazowazuia kutoeleza raghba na matlaba yao kwa uwazi, kwa kuwa nimeshaeleza sana kuhusu baadhi ya mambo ambayo ni ya kimaumbile kwa wanawake na wanaume.                        

Kwa ujumla wanaume huwa hawaelezi matlaba yao kwa kuamini kuwa wanawake wanayajua na hivyo hawaoni haja ya kuwaambia. Jambo hilo sio sahihi, kwa sababu kuficha matlaba yako huyafanya mawasiliano na mwenzako kuwa magumu.                        

Pamoja na hivyo, ninakuletea orodha ya baadhi ya mambo ambayo mumeo anayahitaji, hata kama hatokwambia...                        

HESHIMA                        

Anahitaji heshima kutoka kwa mshirika Maridhawa wa maisha yake. Hili ni jambo analolihitaji kwa nguvu zote. Suala la heshima ni miongoni mwa vitu muhimu sana kwake.                        

Heshima hiyo ina maana ya kuzipa umuhimu fikra zake, mawazo yake, matendo yake na hisia zake kupitia mambo mbalimbali unayoyafanya.                        

KUMSTAAJABIA                        

Sambamba na kuheshimiwa, wanaume wote  wanapenda wahisi kuwa wanastaajabiwa (kuwa admired). Lakini kitu muhimu zaidi wanataka wahisi kuwa wanastaajabiwa kwa nia njema na kwa dhati kwa sababu wana rada inayowaonesha kama uhusiano fulani ni wa kweli au la.                         

USUHUBA                        

Mara nyingi mwanaume hupenda kusuhubiana na mwanamke kwenye eneo linalompa changamoto ili aweze kushinda... Hata kwenye michezo huwa ni hivyo hivyo                        

RAFIKI MWENYE MVUTO                         

Mwanaume humthamini mwanamke anayejitunza na kujinawirisha kwa ajili yake. Sio lazima awe super model, bali kitendo cha kujipamba na kujiremba kwa ajili yake kitamvutia. Hivyo, zitunze nywele zako, kuwa makini na make up yako na mavazi yako.                         

SAUTI YENYE KUBEMBELEZA

Mwanaume anapenda sauti tamu iliyojaa upendo. Fanya juhudi kadiri uwezavyo kulifanikisha hilo. Kwa kawaida watu huwasikiliza zaidi wale wanaozungumza kwa sauti yenye kubembeleza.

KUHAMASISHWA NA KUSHAJIISHWA

Mwanaume anapenda kushajiishwa na kuhamasishwa, na hilo analihitaji haswaa. Anapenda kujua kuwa mkewe anamuunga mkono. Hivyo, ni muhimu sana mwanamke amuamini mumewe, kwa maana akihisi kuwa mkewe anamuamini ataweza kuvuka vizuizi na changamoto za aina yoyote.

KUTHAMINIWA NA KUSHUKURIWA

Mwanaume anapenda kuthaminiwa, jambo ambalo wanataka kulisikia na kuliona pia. Neno “shukran” au “ahsante mume wangu” likisindikizwa na tabasamu linaweza likawasilisha hisia zako maridhawa za namna unavyomthamini. Kumbuka kuwa unapothamini juhudi na kazi zake itamfanya aongeze bidii na kujituma zaidi. Miongoni mwa njia bora kabisa za kuonesha kuwa unathamini juhudi anayoifanya katika kukuhudumia ni kutofuja pesa anazozihangaika na kuepuka matumizi ya hovyo na yasiyokuwa ya lazima, sambamba na kuishi ndani ya uwezo wa bajeti ya mumeo.

KUJALI

Wanaume hufanya mambo mengi kwa ajili ya kuwasaidia marafiki zao na familia  zao pia. Ukilitaja mambo hayo anayoyafanya atajua kwamba unatambua thamani yake katika maisha yenu.

UHURU
Mwanaume anapenda mkewe ampe uhuru. Hiyo haina maana kwamba anataka kukaa peke yake muda wote, bali anapenda ahisi kuwa ana uwezo wa kuendesha na kupangilia mambo yake kwa uhuru bila kuchunguzwa na mkewe au kumfanya ahisi kuwa ni mwenye makosa. Mpe fursa ya kutoka na marafiki zake mara kwa mara au kukaa peke yake katika baadhi ya nyakati.

KUMUUNGA MKONO

Watu wote wanahitaji kuungwa mkono. Mwanaume anapotaka kufanya jambo fulani au mradi fulani muunge mkono. Mfanye ahisi kuwa uko pamoja naye, ahisi kuwa utashikamana naye bila kujali changamoto zozote zitakazomkuta. Muoneshe kuwa lengo lake ndio lengo lako.

Utafika mbali katika ndoa yako ikiwa utakuwa shabiki namba moja wa mumeo. Wakati watu wakifanya kazi ya kumuangusha, wewe fanya kazi ya kumpandisha na kumfikisha kileleni.

KUMPENDA NA KUMHITAJI

Hata kama unaamini kwamba anajua kuwa unampenda, muoneshe kwamba unampenda. Wanaume wanapenda wahisi kuwa wanapendwa au wanahitajiwa na wanawake, jambo ambalo linawafanya wajiamini zaidi. Msifie, mpambe kwa maneno ya kuusifu urijali wake, mpe nyama ya ulimi na umweleze namna anavyokukuna na kwamba una bahati ya kuwa na mume kama yeye.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post