MAMBO USIYOTAKIWA KUFANYA UNAPOENDESHA GARI LA ‘MANUAL TRANSMISSION’

Kuendesha gari la manual sio ngumu sana kama baadhi ya watu wanavyodhani. Pale linapokuja suala la kuendesha gari la manual, ni mchanganyiko wa usanii na sayansi ya mikono na miguu kwa pamoja.
Pale unapoendesha gari ya manual ile gear lever inawezekana ikawa kama kitu kigumu kwako, lakini unapoizoea ni kitu cha kufurahisha na starehe kucheza nacho hasa unapokuwa barabarani. Kuna baadhi ya mambo ya kuzingitia kabla au hata baada ya kujua kuendesha gari ya manual ili kujiweka salama barabarani na kukilinda chombo chako.
Kamwe usitumie gear lever kama egesho la mkono wako
Tunaiona gear lever na kuitumia bila kujua nini kinafanyika nyuma ya pazia. Pale tunapotumia gear lever kubadilisha gear, selector fork ambayo huwa haizunguki huwa inakandamizwa kwenye collar inayozunguka na ile collar huwa inagandamizwa kwenye gear plate unayotaka kubadilisha. Kuweka mkono kwenye gear lever kwa muda mrefu kunasababisha kusagika kwa ile selector fork taratibu na kupunguza urefu wa maisha yake.
Usikanyage Clutch wakati gari linapoteremka katika mteremko ili kuongeza mwendo
Kukanyaga clutch wakati gari linateremka kwa kasi mteremkoni sio jambo la kufanya wakati unaendesha gari la manual. Hii itachangia sana kusaga baadhi ya maeneo katika mfumo wa gear wa gari lako. Pia itapelekea gari lako kukosa balance wakati wa kushuka katika mteremko. Cha kuzingatia ni makadirio ya mwendokasi, gear uliyopo na muda wa kuachia clutch husika.
Usiweke mguu wako muda wote juu ya pedeli ya Clutch
Kukanyaga pedeli ya Accelerator (mafuta) mpaka mwisho pale gari lako linapokuwa katika mwendo mdogo sio vizuri kwa sababu kutapelekea kutumia kiasi kikubwa cha mafuta bila sababu. Unashauriwa kukanyaga pedeli yako ya mafuta mpaka mwisho pale tu unapokuwa katika gear za kasi ili kulifanya gari lako litembee katika mwendokasi mkubwa.
Usibadili Gear bila kukanyaga clutch
Clutch inasaidia kutenganisha injini na gear box kila muda inapokanyagwa. Ni muhimu kukanyaga clutch kwanza kabla ya kujaribu kubadili gear yoyote ili kuipa maisha marefugear box yako. Clutch Unit hutumika kusafirisha mzunguko wa injini kutoka kwenye injini kwenda kwenye transmission.
Usibane brake wakati wa kusimama bila ya kukanyaga Clutch
Wakati unapotaka kusimama ni muhimu sana kukanyaga clutch. Cha kuzingatia hapa ni muda wa kubana clutch, jaribu kupunguza mwendo mpaka pale unapoona sasa unahitaji kusimama na hapo unaruhisiwa kukanyaga clutch na kulifanya gari lako kusimama.
Kumbuka Clutch ni kila kitu linapokuja suala la gari za manual, hakikisha umepata mafunzo ya kutosha kabla ya kuanza kutumia gari la manual katika barabara kuu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post