MAMBO USIYOTAKIWA KUYAFANYA UNAPOENDESHA GARI LA ‘AUTOMATIC TRANSMISSION’

SHARE:

Kila siku teknolojia inakua kwa kiwango kikubwa na imekuwa na manufaa mengi kwa wanadamu. Ukuaji wa teknolojia umepelekea urahisi katika ...

Kila siku teknolojia inakua kwa kiwango kikubwa na imekuwa na manufaa mengi kwa wanadamu. Ukuaji wa teknolojia umepelekea urahisi katika kufanya mambo magumu kuwa mepesi. Hili limechangia katika kupunguza muda na nguvu iliyokuwa ikitumika hapo awali katika kufanya jambo hilo hilo kwa kutumia nguvu kubwa.
Kwa upande wa magari, teknolojia imetuwezesha watu wengi kupata urahisi katika uendeshaji wake kwani magari ya saa ‘automatic’ yamerahisishwa sana tofauti na magari ya manual ambayo yalikuwa yakiwatatiza watu wengi, hasa wanawake.
Kuna tofauti kubwa sana ya kiutendaji kati ya magari haya ya automatic na yale ya manual. Magari haya ya automatic ni rahisi sana kuyaendesha kwa kuwa sehemu kubwa ya mfumo wa utendaji wake ni wa kisasa kabisa na kujiendesha wenyewe. Ila kuna vitu vya msingi usivyotakiwa kufanya wakati unaendesha magari haya ili kuongeza maisha ya gear box (Transmission Box).
Usipaki gari lako bila kuweka Parking Brake (hand brake)
Mara nyingi madereva wamekuwa wakipaki magari yao kwa kuweka gear leaver kwenye herufi P, bila ya kuengage Parking Brake (wengi tunifahamu kama hand brake). Kama wewe ni mmoja wao tafadhali acha kufanya hivyo kwa sababu ‘Parking Pawl’, kichuma kinachoizuia gari kuondoka wakati imewekwa kwenye Park ni kidogo sana na hakijatengenezwa kwa kazi hiyo. Hivyo ikitokea mtu akaligonga gari lako kidogo kuna uwezekano mkubwa wa gari lako likaanza kutembea kama ulikuwa hujalizima. Pia kipande cha Parking Pawl kilichovunjika kinaweza kikaleta matatizo makubwa katika gear box yako.
magari ya sasa yamekuwa na parking brake zinazotofautiana. hizi ni baadhi ya aina tofauti za parking brake.


Usibadili Gear ya mbele ‘D’ kwenda ya nyuma ‘R’ moja kwa moja au ya nyuma kwenda ya mbele moja kwa moja bila ya kusimamisha gari kwanza
Simamisha gari lako kabisa kabla ya kuamua kubadili gear ya kutoka mbele na kurudi nyuma au vinginevyo. Kufanya hivyo bila kusimamisha gari lako kutapelekea uharibifu mkubwa katika gear box yako.
Hakikisha engine inapata joto la kutosha kabla ya kuanza kuendesha gari lako
Kama ulilzima gari lako kwa muda mrefu sana ni bora ukaliacha kwa muda baada ya kuliwasha ili engine ipate joto la kutosha na kufanya vimiminika vyote katika gari kutawanyika na kufika katika maeneo husika katika kiwango stahiki. Hii italifanya gari lako lidumu kwa muda mrefu na itakupunguzia garama ya kufanya marekebisho mara kwa mara.
Usiweke gia ya neutral ‘N’ unapokuwa katika foleni
Madereva wengi wa magari ya automatic wamekuwa na dhana ya kuweka neutral ‘N’ wanaposimama kwenye foleni au kwenye taa za kuongezea magari, wakidhani kuwa wanaokoa kiwango cha mafuta kitakachotumika. Kwa kawaida magari ya automatic yametengenezwa kwa namna ambayo huyawezesha kuokoa kiasi kikubwa cha mafuta. Hivyo ukiiacha kwenye gear ‘D’ haitotumia mafuta zaidi.
Gari inapokuwa katika neutral mzunguko wa injini hupungua, hivyo taa zinaporuhusu ama foleni kuanza kutembea na dereva akaweka gear ya Drive ‘D’ gari inakuwa imepungukiwa na kiwano cha mafuta kilichokuwa kikiingia kaika injini. Ni sawa na kumuamsha mtu usingizini na kumuamuru akimbie mara moja.
Usibadili Gear wakati mzunguko wa engine ya gari ni mkubwa 
Madereva wengi wamekuwa na tabia ya kubadili gear kutoka Drive D na kuweka neutral N wanapokuwa katika mteremko kwa lengo la kuokoa kiwango cha mafuta kitakachotunika. Hii ni hatari sana kwani mhukufanya dereva kushindwa kulihimili gari kwa usahihi. Vilevile kubadili gear wakati mzunguko wa engine ya gari lako ni mkali ni kitu kibaya kwa sababu itasababisha kulika kwa clutch plates za ndani ya gear box yako na kukuletea matatizo hapo baadae.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAMBO USIYOTAKIWA KUYAFANYA UNAPOENDESHA GARI LA ‘AUTOMATIC TRANSMISSION’
MAMBO USIYOTAKIWA KUYAFANYA UNAPOENDESHA GARI LA ‘AUTOMATIC TRANSMISSION’
https://4.bp.blogspot.com/-UH8KBLX0_Kc/WSBLe7vGFQI/AAAAAAAAbmY/K41lsqDfCichH36HNpL3hmv414vxcrtDQCLcB/s1600/xMTAT_2-750x375.jpg.pagespeed.ic.w-5RtIPxpI.webp
https://4.bp.blogspot.com/-UH8KBLX0_Kc/WSBLe7vGFQI/AAAAAAAAbmY/K41lsqDfCichH36HNpL3hmv414vxcrtDQCLcB/s72-c/xMTAT_2-750x375.jpg.pagespeed.ic.w-5RtIPxpI.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/mambo-usiyotakiwa-kuyafanya.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/mambo-usiyotakiwa-kuyafanya.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy