MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU MELI YA RMS TITANIC

Ni meli kubwa ya kihistoria iliyotengenezwa miaka ya 1912 na kufanya kazi kwa siku tano tu toka izinduliwe.najua unaijua ila nataka nikujuze zaid.

-Ilikuwa na urefu wa mita 265 kwa lugha nyepesi ni kama viwanja viwili na nusu na zaidi[​IMG][​IMG]

- Ilikuwa inatumia tani 600 za makaa ya mawe kwa siku yani kwa lugha nyepesi ni kama semi trela 30 na ambapo majivu tani 100 kila siku yalimwagwa baharini na akihitaji watu 176 kwa ajiri ya shughuli ya kuweka makaa ya mawe[​IMG]

-ilitengenezwa kwa muda wa miezi 26 ambapo kulitokea na majeruhi 246 na vifo viwili katika kipindi chote[​IMG]

- kati ya wafanyakazi 885,,,,,,23 tu walikuwa wakike
- mbwa walikuwa 9 ila wawili waliokolewa[​IMG]
- Mwaka 1898 yani miaka 14 kabla ya ajali kuna kitabu kilitungua kiliitwa 'unsinkable' ambacho kiliadithia kuwepo kwa meli kubwa ambayo baadae ikigonga mwamba wa barafu na ile hadithi kwa asilimia 80 iliendana na kilekilichotokea kwenye titanic..mpaka leo kuna watu wanajiuliza kuna uhusiano gani kati ya kile kitabu na meli ya titanic[​IMG]

-Tarehe 16 april 1912 yani siku moja baada ya kutokea kwaajali hiyo,gazeti la 'THE BRITISH NEWSPAPER' ililipoti titanic imezama lakini hamna mtu aliekufa...(ila ni kwa kutokuwa na taarifa kamili)[​IMG]

- Edward smith ndo alikuwa kaptain mkuu wa meli hiyo na ndio ilikuwa safari yake ya mwisho ili astaafu kazi hiyo lakini alizama chini na meli[​IMG]

- inakadiliwa kaptain alieripoti mwamba ule, angewahi kulipoti sekunde 30 tu kabla alivyolipoti ajali isingetokea

- life boat nyingi za kuokoa watu zilibeba watu pungufu ya uwezo wake..kuna moja ilibeba 12 ambapo ilikuwa na uwezo wa kubeba watu 40 kutokana na kugombania[​IMG]

-baada ya kuzama tarehe 15 april 1912 meli ikapatikana miaka 73 baadae[​IMG][​IMG][​IMG]

- miili 336 pekee ndo ilipatikana kati ya miili 1514 ya waliofariki[​IMG]

- iligonga mwamba saa tano na dakika arobain usiku na ikazama baada ya masaa 2 na dakika 40 

- meli ya californian iliitangulia meli ya titanic kwa masaa kadhaa lakin ilisimama baada ya kuona hali ya bahari sio nzuri...lakini titanic ikaipita califonian..na californian ikatuma jumbe za taadhari kwa titanic lakin titanic wakazipuuzia kwakuamin titanic ni 'unsikable' 

- baada ya mda titanic ilipopata ajali ikatuma jumbe za msaada kwa carlifonian lakin kwa bahat mbaya mtu wa kushughulikia mawasiliano usika alikuwa ameshalala ambapo meli hyo ingeokoa mamia ya watu

- ndo siku anazaliwa mwanzilishi wa taifa la korea kaskazin kim II sung[​IMG]

- ndio meli pekee iliyozama kwa kugonga mwamba wa barafu mpaka sasa

- kati ya watu 711 waliookolewa, wanaume walikuwa pungufu ya seruthi

-mhanga wa mwisho wa ajali hiyo alifariki mwaka 2009 may 31,akiwa na umri wa 97 na alikuwa na umri wa miezi miwil tu wakat wa ajali

- sheria nyingi za usalama wa watu bahari zilianzishwa baada ile ajali..

mwishoni napenda kutoa changamoto kwetu hapa nyumbani tz hatuna utaratibu wa kuweka kumbukumbu za vitu kama hivi kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo..mi kiukwel ukinambia kuhusu mv bukoba ajali yake siijui vizuri maana nahisikia juu juu tu...hata kwa upande wa michezo..leo hii ningependa kusikia mbwana samata amevunja rekodi iliyowekwa na mchezaji fulan mwaka 1970 kwa kufunga mabao mengi kwenye timu ya taifa lakin hakuna.


makala hii kwa hisani ya JF
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post