MAMBO YA KUFANYA UNAPOKOSA HAMU YA KUJAMIIANA

SHARE:

Watu wengi wamekuwa wakikumbwa na tatizo la ama kupata hamu ya kujamiiana inayoisha kwa muda mfupi ama kukosa kabisa hamu ya kujamiiana. ...

Watu wengi wamekuwa wakikumbwa na tatizo la ama kupata hamu ya kujamiiana inayoisha kwa muda mfupi ama kukosa kabisa hamu ya kujamiiana. Utakuta mwanaume anahitaji kupata tendo la ndoa lakini mwanamke anakuwa hana hamu ama mwanamke ana hamu na wakati huo huo mwanaume wake hana hamu kabisa.
Tatizo hili limekuwa likiwaathiri watu wengi hapa nchini na hata duniani kote. Haliwaathiri wanaume pekee, bali hata wanawake nao hukumbwa na tatizo hilo.
Utafiti uliofanyika nchini Uingereza , Ulaya na Marekani, ukijumuisha wanawake wa rika zote, ulibaini kuwa asilimia kati ya 30 na 50 ya wanawake wanakumbwa na tatizo la kukosa hamu ya kujamiiana.
Wakati huo utafiti huo ukiweka bayana hilo kutokana na tatizo la uzazi au kukoma kwa hedhi, tafiti nyingne zinaonyesha kuwa karibu robo tatu ya wanawake hawafikii kilele cha tendo hilo au wanapata maumivu.
Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa kukosa hamu ya tendo la ndoa kunatibika, iwapo hatua muhimu na za msingi zitachukuliwa.
Ni vyema kufika mapema katika huduma za afya ukiwa na mwenza wako kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Kwanza kabisa, inashauriwa kitaalamu kubadilisha mfumo wa maisha kwa mfano, kubadili ratiba za kazi, matembezi au ratiba za wenza.
Kingine ni kufanya mazoezi mara kwa mara kwa sababu mazoezi huongeza ufanisi, lakini pia kupunguza uzito na humfanya mtu kuwa na umbile zuri, furaha na kuongeza ufanisi wakati wa kujamiiana.
Kupunguza msongo wa mawazo kwa kukubali kwamba tatizo lipo baina ya wanandoa na hivyo kutafuta suluhu pamoja na kuacha ugomvi. Matatizo ya kimaisha lazima yatafutiwe ufumbuzi.
Kufanya mazoezi ya misuli ya kiuno kwa kufanya kama unazuia mkojo wakati unahisi haja ndogo na kuhesabu kutoka moja hadi tano, baada ya tano pumzika na halafu rudia. Haya mazoezi (kegel exercise) huongeza uwezo wa kujamiiana kwa wanawake.
Kubadilisha mfumo wa maisha kwa wapenzi
Zungumza na mwenza wako – Malumbano na matatizo ni vitu vya kawaida katika uhusiano wowote, ni vizuri kwa wenza kukaa pamoja na kuzungumza matatizo yao, kuwa wa kweli, waaminifu, kuaminiana, kujaliana na kuzungumza juu ya tendo la ndoa kwa pamoja.
Ni vizuri kila mmoja kuainisha vitu anavyopenda na asivyopenda kufanyiwa wakati wa kujamiiana. Pale inapotokea mmoja hajapendezwa au kufurahishwa na uwajibikaji au ufanisi wa mwenzie basi hana budi kutumia lugha nzuri kutafuta kiini cha tatizo na kulitafutia ufumbuzi.
Weka mazingira mazuri na muda wa kufanya tendo la ndoa na mwenza wako ili mpate kudumisha uhusiano wenu.
Ongeza msisimko katika uhusiano wenu kwa kujaribu aina au staili mbalimbali wakati wa kujamiiana, kubadilisha muda wa kufanya mapenzi (sio usiku tu hata asubuhi, mchana) au sehemu tofauti na ile mliyoizoea wakati wa kufanya mapenzi (sio kila siku kitandani).
Kupata ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa mambo ya uhusiano, ndoa na hata madaktari wa magonjwa ya akili kwani hawa ni weledi zaidi katika kazi yao.
Tiba ya dawa
Kutibu ugonjwa ambao ni kiini cha tatizo hili – Kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya zinaa nk. Daktari kumbadilishia mgonjwa dawa zinazosababisha madhara kama ya msongo wa mawazo na sonona.
Kutibu tatizo la sonona na wasiwasi.
Kutumia dawa au vilainishi vya ukeni wakati wa tendo la ndoa kwa wale wanaopata maumivu au kupunguza uke kuwa mkavu au kuwasha.
Tiba ya vichocheo (homoni)
Dawa za kitaalamu za kuongeza hamu au nguvu atakuandikia daktari baada ya kufahamu kiini cha tatizo. Haishauriwi kutumia bila ushauri wa daktari kwani dawa hizi zina madhara.
Vyakula vinavyosaidia kupunguza tatizo hili
Ikumbukwe ya kwamba vyakula hivi sio tiba mbadala bali husaidia tu kupunguza ukubwa wa tatizo hili la kupungua au kukosa hamu ya kujamiiana na kuboresha kwa wale ambao hawana tatizo hili na hivyo kudumisha uhusiano.
Kitunguu swaumu – Kitunguu swaumu kina kemikali ambayo huongeza mzunguko wa damu kwenda kwenye uume, huongeza hamu ya kufanya mapenzi na utolewaji wa mbegu za kiume.
Habat al soda – Mafuta, mbegu, au unga wa habat soda kama wengi wanavyoiita na ambazo zimetumika kwa miaka mingi sana kupunguza tatizo hili na waandishi wengi wa tiba ya nguvu za kiume wameeleza umuhimu wake. Tumia kidogo kwenye chai au maji ya uvuguvugu mara mbili kila siku. Mbegu hizi hupatikana kwa wingi katika nchi za asia kama Saudi Arabia, Syria, Iran, Dubai (UAE), na hata Misri, Tanzania­ maeneo ya pwani hupatikana.
Giligilani – Hii huchochea hamu ya tendo la ndoa kutokana na uwepo kwa wingi wa kichocheo aina ya androsterone.
Ndizi – kuwepo kwa wingi kwa kimeng’enyo aina ya ‘bromelain’ na madini ya potashiam, huongeza msisimko wa tendo kwa wanaume. Potassium pia hupatikana kwenye tikiti maji ambalo pia lina kemikali aina ya ‘arginine’ ambayo huongeza wingi wa damu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kusimika kwa uume.
Parachichi – Huwa na kiwango kikubwa cha madini ya folic acid ambayo huvunjavunja protini. Vitamini B6 kwenye parachichi huchochea kutengeza vichocheo vya kiume kwa wingi.
Mayai – Mayai yana kiwango kikubwa sana cha vitamini aina ya B5 na B6, ambazo husaidia kuleta usawa wa viwango vya vichocheo mwilini na kupunguza msongo wa mawazo.
Nyanya – Zina kiwango kikubwa cha virutubisho aina ya bio­active phyto­nutrients, lycopene, na beta carotene ambazo husaidia kuleta damu kwa wingi kwenye uume na hivyo kusaidia kusimika kwa uume
Chocolate – Ina kiwango kikubwa cha kemikali ambazo huongeza hamu ya tendo. Vitamin A – Husaidia katika kuweka usawa wa vichocheo vya mapenzi.
Vyakula venye wingi wa vitamin hii ni pamoja na karoti, maini,tikiti maji, spinach, maziwa nk. Vitamin B complex – Huongeza kiwango cha kichocheo cha testerone ambacho husaidia katika kuongeza ufanisi wa tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake.
Vitamini B complex hupatikana kwa wingi kwenye ndizi, viazi tamu, lentils mboga za majani, parachichi, mayai, samaki aina ya jodari (tuna), bata mzinga, maini nk. Mdalasini na Asali– Mchanganyiko wa vitu hivi viwili husaidia sana katika kuongeza ufanisi kwa wale wenye tatizo hili.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAMBO YA KUFANYA UNAPOKOSA HAMU YA KUJAMIIANA
MAMBO YA KUFANYA UNAPOKOSA HAMU YA KUJAMIIANA
https://4.bp.blogspot.com/-2mkgbZZlgmo/WR9XvTf1R7I/AAAAAAAAbi0/JDoWuMeNJJcqywxE8qaM0wBsrz79CaleACLcB/s1600/x3a13cfbd-00ed-4238-bd9e-f4004e72eb46-750x375.jpg.pagespeed.ic.kkvqkEiHrZ.webp
https://4.bp.blogspot.com/-2mkgbZZlgmo/WR9XvTf1R7I/AAAAAAAAbi0/JDoWuMeNJJcqywxE8qaM0wBsrz79CaleACLcB/s72-c/x3a13cfbd-00ed-4238-bd9e-f4004e72eb46-750x375.jpg.pagespeed.ic.kkvqkEiHrZ.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/mambo-ya-kufanya-unapokosa-hamu-ya.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/mambo-ya-kufanya-unapokosa-hamu-ya.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy