MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAWATAHADHARISHA WAKAZI WA MIKOA YA PWANI

Mamlaka ya usimamizi wa hali ya hewa nchini imetoa angalizo kwa wakazi wa mikoa ya mwambao wa Pwani kuwa mvua kubwa zitaendelea kunyesha hivyo waweze kuchukua tahadhali mapema.
Aidha, Mamlaka hiyo imesema kuwa mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya unguja na Pemba vinatarajiwa kuwa na mvua kubwa inayoambatana na upepo pamoja na mawimbi makubwa.
Taarifa hiyo imesema kuwa hali hiyo inasababishwa na kuimarika kwa ukanda wa mvua nchini na kusababisha kuwepo kwa mgandamizo mkubwa Bahari ya hindi ambayo inasababisha kuwepo kwa mvua kubwa katika ukanda huo.
Hata hivyo, Mamlaka ya hali ya hewa imewataka wakazi wa maeneo husika kuwa na tahadhari pia kuchukua hatua stahiki pindi wanapoona hali isiokuwa ya kawaida.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post