MANISPAA YA IRINGA YAANZA KUTENGENEZA BARABARA MBOVU YA MTWIVILA SEKONDARI

manispaa ya  Iringa  imeanza  kutengeneza barabara ya Mtwivila  sekondari  japo  changamoto  kubwa ya barabara   hiyo ni mifereji ya maji  ya  mvua  ndio  huwa inachangia  ubovu wa  barabara hii
NITAKUWA  wa kwanza  kuipongeza halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  iwapo utengenezaji wa barabara  hii ya Mtwivila sekondari ukaenda  sanjari na ujenzi  wa  mifereji ya maji ya mvua vinginevyo sitanyamaza kimya kuona  mamilini ya  kodi za  wnanchi  yanatumika kutengeneza  barabara  ambazo tunajua wazi  baada ya mvua  zitaharibika  kwa  kukosa mifereji ya maji  ya mvua.
Nimekuwa wa kwanza kusema  hili kwani  sitamani  kuona  kilichotokea  Gangilonga kwa  barabara ya shule ya Msingi Mapinduzi kutokea  Mtwivila  Sekondari utengenezaji wa  barabara ya Mapinduzi kweli kuna haja ya Manispaa kwenda  kujionea kama ndivyo walivyokubaliana maana  sio kabisa .
Leo najitolea kufuatilia   hatua kwa  hatua ya barabara  hii ya Mtwivila  sekondari wakifanya  vema  nitapongeza  wakifanya ovyo ovyo   sita nyamaza  kimya .
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post