MARCUS RASHFORD AIPATIA MANCHESTER UNITED USHINDI UGENINI

Mpira wa adhabu uliopigwa kiufundi na mchezaji kijana Marcus Rashford umeipatia Manchester United nafasi ya kushinda mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya mchezo wa Ligi ya Uropa dhidi ya Celta Vigo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 aliupiga mpira huo kwa kuuzungusha na kuifanya United, sio tu iongoze bali pia kupata goli lenye thamani la ugenini kabla ya kurudiana katika dimba la Old Trafford Alhamisi ya wiki ijayo.

Mnchester United ikiwa ipo nje ya nafasi nne za juu za Ligi Kuu ya Uingereza ikiwa pointi moja nyuma ya Manchester City, kushinda Ligi ya Uropa ndio kunaweza kuwa ndio nafasi pekee kwake kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Kipa wa Celta Vigo akijaribu bila mafanikio kuuzuia mpira wa adhabu uliopigwa na Marcus Rashford
 Kiungo wa bei mbaya wa Manchester United Paul Pogba akianguka vibaya wakati alipochuana na mchezaji wa Celta Vigo

   Kocha Jose Mourinho akitupa chini note book yake na kalamu ili afuatilie vizuri mchezo wa jana
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post