MAREKANI YASITISHA MSAADA NCHINI KENYA

Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) limesitisha misaada katika sekta ya afya nchini Kenya kutokana na tuhuma mbalimbali za rushwa.
“Tumechukua hatua hizo kutokana na uwepo wa vitendo vya rushwa, pamoja na kutokuwapo njia madhubuti za matumizi ya fedha katika wizara,”  ilieleza taarifa hiyo ya USAID.
Aidha, shirika hilo limetanabaisha kuwa uamuzi wa kusitisha misaada hiyo ni ili kuweza kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa na kodi ya raia wa Marekani zinawafikia walengwa.
Mwaka uliopita, mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini Kenya alisema jumla ya dola 50 milioni hazikubainika zilivyotumiwa katika wizara ya afya.
Maafisa wakuu katika wizara ya afya pamoja na jamaa za baadhi ya viongozi wakuu serikalini walidaiwa kuhusika katika kufujwa kwa pesa hizo.
Kwa mujibu wa ubalozi wa Marekani nchini humo, umesema kuwa unafanya kazi kwa karibu na wizara kuweza kuhakikisha wanapata misaada pale ambapo vitendo vya rushwa juu ya fedha hizo vitakapokomeshwa.
Hapa chini ni taarifa iliyotolewa na shirika hilo;

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post